Mtetezi wa demokrasia Agnes Chow aachiliwa huru Hong Kong

0



Mwanaharakati wa demokrasia Agnes Chow ameachiliwa huru leo baada ya kutumikia kifungo cha miezi saba jela kwa makosa ya kushiriki maandamano haramu ya kuipinga serikali mjini Hong Kong mwaka 2019. Mwanaharakati huyo aliye na miaka 24 alitiwa hatiani pamoja na mwenzake wa kiume Joshua Wong, kwa kushiriki maandamano hayo yaliofanyika karibu na makao makuu ya polisi katika mji huo unaotawaliwa na China. Wong bado yupo jela na sababu ya kuachiliwa mapema kwa Agnes Chow aliyepaswa kutumikia kifungo cha miaka 10 jela, bado haijajulikana. Baada ya kuachiwa huru Chow hakuzungumza na waandishi habari, aliingizwa haraka ndani ya gari na kuondoka pamoja na wanaharakati wenzake watetezi wa demokrasia mjini Hong Kong.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable