Putin anatumai Biden ni muelewa zaidi kuliko Trump

0



Rais wa Urusi Vladimir Putin ameelezea matumaini yake kuelekea mkutano kati yake na Rais wa Marekani Joe Biden akisema anatumai Biden atakuwa muelewa zaidi kuliko mtangulizi wake Donald Trump. Katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la NBC, Putin alimuelezea Biden kama mtu aliye na uzoefu mkubwa wa kisiasa. Licha ya kukiri kuwa mahusiano kati ya mataifa hayo mawili yamedorora amesema anatumai ataweza kufanya kazi vizuri na Biden. Biden anapanga kujadili masuala muhimu na Putin ikiwemo Urusi kuuingilia uchaguzi wa Marekani pamoja na udukuzi wa mtandaoni katika mkutano wao unaotarajiwa kufanyika Jumatano wiki Ijayo mjini Geneva. Putin alisema wazi kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2016 alimuunga mkono rais wa zamani Donald Trump kuwa rais wa Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable