Mwendesha mashitaka mkuu mpya wa ICC aanza rasmi kazi

0


Muingereza Karim Khan ameanza kazi leo ya mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC akikabiliwa na mrundiko wa kesi ikiwemo uchunguzi wa mashambulizi ya Israel na Palestina, ikiwa ni kesi kubwa kabisa ya kisiasa katika historia ya mahakama hiyo. 

Khan anachukua mikoba ya Mgambia Fatou Bensouda, ambaye alipanua wigo wa mahakama hiyo wakati wa muhula wake wa miaka tisa lakini akakabiliwa na msururu wa matukio makubwa ya kushindwa, ikiwemo kufutiwa mashitaka aliyekuwa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo.

 Khan mwenye umri wa miaka 51, ambaye alichaguliwa na nchi wanachama wa ICC Februari mwaka huu kuwa mwendesha mashitaka wa tatu mpaka sasa wa mahakama hiyo pekee ya kudumu ulimwenguni ya uhalifu wa kivita, ameapishwa leo katika hafla iliyoandaliwa katika makao makuu ya mahakama hiyo mjini The Hague.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable