Nyembe maarufu chapa ya Alshabab zatia hofu mamlaka za Msumbiji

0

 


Wembe wa chapa ya jina sawa na kundi la wanamgambo wa kiislamu ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi dhidi ya wakazi wa mji wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji, limeshtua mamlaka.

Wembe wa chapa ya Alshabab umaarufu wake ulikuwa ukiongezeka mwaka jana.

Hivi sasa mamlaka zina hofu kuwa kuna uhusiano wa bidhaa hiyo na wanamgambo.

Mkuu wa polisi, Bernardino Rafael, sasa ameamuru maafisa kukusanya taarifa kuhusu wembe chapa ya alshabab kuona kama ni sehemu ya propaganda ya wanamgambo.

Masoko ya manispaa ya mji wa Pemba, huko Cabo Delgado, yamekuwa yakiunza nyembe hizo tangu mwaka hana, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo.

Bidhaa hiyo iligundulika makao makuu ya Msumbiji, Maputo, na sasa inauzwa katika jimbo la Manica. Ripoti zimeeleza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable