Waziri Uganda aamuru wanaokiuka miongozo ya kupambana na corona wachapwe viboko

0

Waziri Uganda aamuru wanaokiuka miongozo ya kupambana na corona wachapwe viboko





Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu , Dkt Monica Musenero, ametoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya wa Butebo, Bw. Emmy Mitala, kuwachapa viboko raia watakaokiuka miongozo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona nchini hum. Gazeti la Daily Monitor limeandika.

''Wachape tu kama hawasikilizi. Ninatoa maelekezo haya kama mwenyekiti mwenza wa timu ya utekelezaji, usiruhusu watuhangaishe. Nilikuta duka la Petete likiwa limejaa watu, wakiwemo watoto, kama vile hakuna sharti la kusalia nyumbani,'' alisema Dkt Musenero.

Waziri huyo ametoa maelekezo hayo wakati wa mazishi ya mama mmoja wa miaka 81 Eunice Logose Shaine katika kijiji cha Kabelekeke Village mwishoni mwa juma.

Musenero alilazimika kutoa amri ya kuchapa viboko kwa wakazi hao baada ya Mkuu huyo wa Wilaya Emmy kulalamika kuhusu kuendelea kukiuka maagizo ya rais hatua ambayo imeongeza kasi ya kuenea zaidi kwa virusi vya corona gazeti la Independent limeripoti nchini humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable