Samia: Kazi ya urais ni ngumu

0

 




Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema bila kazi ya urais ni ngumu lakini kwa ushirikiano wa taasisi za Serikali pamoja na wanahabari anaamini atafanikiwa.

“Labda niwaambie bila kupepesa kazi ya urais ni ngumu lakini kwa sababu  urais ni taasisi yenye vyombo kadhaa vinavyosaidia ndipo urahisi wake ulipo. Rais afanye kazi peke yake kama mnavyojua Serikali ina sekta kadhaa ambayo kila linalozuka linashughulikiwa.”

“Rais anapelekewa aidha kwa maelekezo au kwa  uamuzi, lakini ndani ya ofisi ya rais kuna wasaidizi kadhaa wanaosaidia kuchakata na kukupa kwa ajili ya uamuzi. Lakini niseme sio rahisi ki hivyo kwa sababu lazima ujue kila kitu kinachotokea au kilichopo ndani ya nchi ili kinapokuja kisiwe kigeni kwako,” amesema Rais Samia.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ameeleza hayo leo Jumatatu Juni 28, 2021 katika mkutano wake na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Katika ufafanuzi wake amesema kazi ya urais lazima usome na kwa siku moja mafaili yanayoingia ofisini kwake ni kati ya 30 hadi 25 na lazima ayapitie.

Amebainisha kuwa kazi ya urais ni ngumu na ugumu unakuja endapo  kama hukujiandaa  kuichukua lakini ukijitayarisha, kuchukua na kujaza fomu na kupiga kampeni unakuwa na  uhakika ya kukabiliana na yale utakayoyakuta.

“Lakini kwa upande wangu nilizunguka na kupiga kampeni na kushawishi watu watuchague nikijua nina bonge la kaka juu yangu hapa (Hayati John Magufuli) atabeba mimi nitakuwa nikisaidia. Kwa mapenzi ya Mungu limetokea la kutokea ule mzigo umekuja mabegani kwangu, sikupata uzito wa kuupokea kwa sababu nilikua najua kilichomo.”

“Nilikuwa najua tumeahidi nini kwa wananchi, tumejipanga kuwatumikia wananchi lakini kulifanya kama wewe lina ugumu wake. Hata hivyo ninawathibitishia kuwa ninaweza kwenda nalo, nina usaidizi wa taasisi zote lakini kwa ushirikiano wenu wanahabari kwa pamoja tutafika,” amesema.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable