Homebongo habariSerbia na Kosovo kuanza tena mazungumzo Serbia na Kosovo kuanza tena mazungumzo 0 ben June 15, 2021 Serbia na Kosovo kuanza tena mazungumzoViongozi wa Serbia na Kosovo wako mjini Brussels leo kuanza tena mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Ulaya yanayonuiwa kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa muda mrefu kuhusu mipaka barani Ulaya. Mkutano wa leo ni wa kwanza tangu Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti kushinda uchaguzi wa bunge mwezi Februari, akiahidi kuchukua muelekeo mpya kwenye mazungumzo hayo na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic. Mkuu wa Sera ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell amesema mdahalo huo hautakuwa rahisi, lakini akahimiza kutumia fursa iliyojitokeza kutokana na ari mpya ya Ulaya kuhusu mazungumzo baina ya nchi hizo jirani za eneo la Balkan. Mazungumzo kati ya Serbia na Kosovo yanafanyika wakati Rais Joe Biden wa Marekani akitarajiwa kukutana na wakuu wa Umoja wa Ulaya, lakini hakuna dalili endapo atakutana na viongozi wa nchi hizo mbili. Tags bongo habari Newer Older