Homebongo habariUmoja wa Mataifa wataka uchaguzi huru na wa haki Mali Umoja wa Mataifa wataka uchaguzi huru na wa haki Mali 0 ben June 15, 2021 Umoja wa Mataifa wataka uchaguzi huru na wa haki MaliUmoja wa Mataifa umetowa wito wa kuitishwa uchaguzi huru na wa haki nchini Mali pasipo viongozi wa sasa wa mapinduzi ya kijeshi kushiriki. Idadi kubwa ya nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja huo ziliutoa mwito huo katika kikao kilichofanyika jana mjini New York. Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Nicola de Riviere amesema kipaumbele kikubwa kinatakiwa kuwa maandalizi ya uchaguzi wa rais tarehe 27 Februari mwakani, akisisitiza kwamba viongozi waliohusika kwenye mapinduzi hawatakiwi kushiriki. Kwa upande wake, naibu balozi wa Marekani katika Umoja huo, Jeffrey DeLaurentis, amesema ni suala la umuhimu mkubwa kwamba uchaguzi wa mwaka ujao uwe huru na wa haki na usimamiwe na mamlaka zenye uwezo kwa kutumia michakato iliyo wazi. Mali ilitangaza serikali mpya huku viongozi wa kijeshi wakishika nyadhifa muhimu, kufuatia mapinduzi yaliyoongozwa na Kanali Assimi Goita mwezi uliopita. Tags bongo habari Newer Older