Simbachawene Atoa Maagizo 6 Kukabili Mihadarati

0

 


SERIKALI imesema itaongeza nguvu  ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya hususani kwa vijana ambao ni nguvu kazi kwa Taifa.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alisema hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  kwenye Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani iliyofanyika jijini Dodoma.


Simbachawene alitoa maagizo sita katika kupambana na dawa za kulevya na kutaka waraibu wa dawa hizo wapewe mitaji baada ya kurudi katika hali zao za kawaida. 


Aliagiza kutoa elimu kwa wanahabari  waweze kutoa mchango mkubwa katika kielimisha wananchi kupitia maandiko na vipindi vya redio na televisheni.


Pia asasi zisizo za kiserikali zinazofanya kazi katika mapambano dhidi ya  dawa za kulevya kutoa elimu  jamii isijiingize kwenye matumizi . 


Maagizo mengine ya serikali ni kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimuna viongozi wa dini kukemea matumizi ya dawa za kulevya.


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolonia imetakiwa kuboresha mitaala   kuwezesha vijana kupata elimu juu  madhara  ya matumizi ya dawa za kulevya. 


Waziri Simbachawene alisema tatizo la matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa huku bangi ikiongoza kwa kuwa na watumiaji wengi ikifuatiwa na heroin na cocaine ambazo huingia kutoka nje ya nchi.


Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Gerald Kusaya alisema Mamlaka imekamata watuhumiwa 12,549 na kati ya hao, 10 ni kuhusiana na cocaine, 605 heroin, 10,282 bangi na watuhumiwa 1,555  ni wa mirungi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable