Wakili: Mshambuliaji wa Wuerzburg huenda akajidhuru

0

 Wakili: Mshambuliaji wa  huenda akajidhuru




Wakili wa umma anayemtetea mwamamume wa Kisomali anayetuhumiwa kufanya shambulizi la kisu mjini Wuerzburg, kusini mwa Ujerumani anadhani kwamba mteja wake anaweza akajidhuru mwenyewe wakati akizuiliwa kizuizini kabla ya kushtakiwa. Wakili Hanjo Schrepfer ameliambia shirika la habari la dpa leo kwamba alichobaini ni kuwa mteja wake anakabiliwa na shinikizo kubwa la kisaikologia. Wachunguzi pia wanakiona kitisho hiki. Msemaji wa ofisi ya kitengo cha polisi kinachoshughulikia uhalifu mjini Munich amesema maafisa wa gereza anakozuiliwa mtuhumiwa wamefahamishwa kuhusu uwezekano wa mshukiwa huyo kujiumiza mwenyewe. Hata hiyo hakusema ni hatua gani za tahadhari zilizochukuliwa na gereza hilo. Mwanamume huyo wa Kisomali anashikiliwa katika gereza la Wuerzburg anakabiliwa na mashtaka 3 ya mauwaji, mauwaji bila kukusudia na kusababisha majeraha mabaya katika mwili yanayohatarisha maisha katika kesi nyengine 6. Wakili Schrepfer amesema anasubiri kuyaona majalada ya uchunguzi haraka iwezekanavyo kabla ya kuzungumza na mteja wake kuhusu kilichotokea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable