Raia wa Iran wanapiga kura kumchagua rais mpya huku mmoja kati ya wagombea wanne akitarajiwa kumrithi Hassan Rouhani ambaye anachukuliwa kama mwenye msimamo mkali.
Kura za maoni zinaonesha kuwa Ebrahim Raisi, kiongozi wa kidini wa Shia ambaye ni mhafidhina anayeongoza mahakama, ndiye anayependelewa kuchukua wadhifa huo.
Aliyekuwa gavana wa benki kuu ambaye anachukuliwa kuwa na msimamo wa wastani Abdolnasser Hemmati ndiyo mpinzani mkuu.
Wapinzani na baadhi ya wanaopendelea mabadiliko wametoa wito wa kususiwa kwa uchaguzi, wakisema kuzuiwa kwa wagombea kadhaa kushiriki uchaguzi huo kumefanya Bwana Raisi kutokuwa na upinzani wa kisawa sawa.
Kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei amepiga kura yake mapema Ijumaa katika mji wa Tehran na kuhamasisha raia kujitokeza kupiga kura.
"Kila kura inahesabiwa ... jitokezeni mumpigie kura na kumchagua rais wenu," alisema. "Hili ni muhimu kwa hatma ya baadaye ya nchi yako,"
Kuna minung’uniko mingi miongoni mwa raia wa Iran kuhusiana na changamoto za kiuchumi ambazo wamekumbana nazo tangu Marekani ilipojiondoa katika mpango wa nyuklia wa Iran miaka mitatu iliyopita na kuwekewa tena vikwazo vilivyolemaza nchi hiyo.
Ushindi kwa mmoja wa wenye msimamo mkali hakutarajiwi kutatiza mazungumzo kati ya Iran na nchi zenye nguvu duniani ambayo lengo ni kuyafufua tena, kulikofanya Iran kukubali kupunguza kasi ya mpango wake wa nyuklia katika sehemu ya mabadilishano ya kuondolewa kwa vikwazo.
Bwana Rouhani, mwenye msimamo wa wastani ambaye alitafuta kufanya majadiliano na nchi za Magharibi, hawezi kuchaguliwa tena kwasababu ameshahudumu kwa mihula miwili ya miaka minne minne.
Ni kina nani walioidhinisha wagombea?
Takriban wagombea 600 wakiwemo wanawake 40, walishiriki zoezi la kutaka kuingia debeni.
Lakini mwisho wa siku ni wanaume saba pekee ndio walioidhinishwa mwezi jana na mahakimu 12 na wanatheolojia wa Baraza la Guardian, bodi yenye kufanya maamuzi kuhusiana na wagombea waliotimiza vigezo vya kugombea.
Eshaq Jahangiri, Bwana makamu wa kwanza wa rais wa Rouhani na Ali Larijani, aliyekuwa spika wa bunge ambaye ni mhafidhina ni miongoni mwa wagombea mashuhuri ambao walifungiwa kugombea.


