Risala za rambi rambi zimeendelea kutumwa kufuatia kifo cha Rais mwamzilishi wa Zambia Kenneth Kaunda, aliyefariki Alhamisi akiwa na miaka 97.
Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi alimwelezea rais huyo wa zamani kama “mpiganiaji ukombozi wa nchi wa hadhi ya juu” kutokana na “ alivyojitolea mhanga kwa maslahi ya sio nchi yake tu bali pia kwa mataifa jirani na ubinadamu kwa ujumla”.
Alisema Kaunda alikuwa ''rafiki wa dhati wa Botswana wakati ilipokuwa inapitia kipindi kigumu'' kutokana na mchango wake katika harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo.
Rais Masisi ametangaza siku saba za maombolezo kwa heshma ya marehemu kiongozi huyo wa Zambia:
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema nchi yake inaomboleza “kifo cha baba wa uhuru na umoja wa Afrika – Rais Kenneth ‘KK’ Kaunda”.
Chama tawala cha African National Congress (ANC), kilimtaja Kaunda kama kigogo wa wa Afrika Kusini na mpiganiaji harakati za ukombozi wa Afrika.
“Dkt Kaunda anashikilia nafasi muhimu katika chama chetu, nchi yetu na watu wa Afrika Kusini. Alitukaribisha Zambia na kuifanya kuwa makao makuu ya ANC kwa zaidi ya miaka 30,” taarifa ya chama hicho ilisema.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema Afrika “mpigania ukombozi, mzalendo na mwanamajumui wa kweli”.
Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo alimkumbuka kama mmoja wa viongozi wa mwisho waliopigania uhuru ambaye alijitolea kwa njia tofauti.
Soma zaidi:

