Ufaransa yatangaza kumuua mshukiwa wa mauaji ya waandishi wake wawili

0


Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly amesema wanajeshi wake wamemuuwa mpiganaji wa Jihadi kutoka Mali aliyedhaniwa kuhusika na utekaji nyara na mauaji ya waandishi wawili wa Ufaransa mwaka 2013. Parly amesema wanajeshi hao walio katika ukanda wa Sahel waliwauwa magaidi wanne wakati wa operesheni yao Kaskazini mwa Mali mnamo Juni 5 akiwemo Bayes Ag Bakabo, mshukiwa Mkuu wa mauaji ya waandishi hao wa kituo cha utangazaji cha Ufaransa cha RFI, Ghislaine Dupont na Claude Verlon. Waziri huyo wa Ulinzi wa Ufaransa ameongeza kuwa Bakabo, alikuwa katika kijiji cha Aguelhok na alikuwa anapanga mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa wakati alipouwawa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable