Umoja wa Mataifa wazungumzia juu maafa ya kukiukwa haki za binadamu Myanmar

0



Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu kuongezeka kwa umwagikaji damu nchini Myanmar inayopitia kipindi cha mgogoro. Kwa mujibu wa taarifa, harakati za kijeshi zinaimarishwa hasa kwenye jimbo la Kayah la mashariki na kwenye jimbo la Chin la magharibi mwa nchi hiyo. Hali hiyo inajiri miezi minne baada ya jeshi kuuangusha utawala wa kiraia. Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet, amesema hayo leo hii. Bachelet amesema Jeshi la Myanmar linatumia ndege na silaha kali kuyashambulia makundi yenye silaha lakini pia kuwashambulia raia. Kamishna huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa kwenye jimbo la Kayah linalopakana na Thailand watu zaidi ya laki moja wamekuwa wakimbizi wa ndani na wengi miongoni mwao wamekwama msituni wakiwa hawana mahitaji muhimu ya kutosha kama maji, chakula na dawa. Wakati huo huo, kiongozi wa serikali iliyoangushwa na jeshi, Aung San Suu Kyi, pamoja na wengine wameshtakiwa kwa makosa mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable