Merkel atahadharisha, corona bado haijaondoka kabisa

0


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametahadharisha kwamba janga la corona bado halijaondoka kabisa licha ya kuridhika juu ya kuundelea kupungua kwa idadi ya maambukizo. Kansela Merkel amesema hatua za kudhibiti maambukizo zilizochukuliwa tangu wakati wa Pasaka zimechangia katika kupungua kwa idadi ya watu wanaoambukizwa lakini amesisitiza tahadhari na amesema kuwa janga la corona bado halijatoweka. Amesema bado pana hatari kutokana na virusi vipya aina ya Delta vilivyobainika nchini India na kuenea pia nchini Uingereza. Shughuli nyingi zimeanza kufunguliwa tena nchini Ujerumani lakini matukio ya kuwaleta pamoja watu wengi bado hayajaruhusiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable