Ushuhuda wa wathirika majaribio dawa ya Ukimwi (2)

0

Kwa mujibu wa waathirika hao, majaribio hayo yaliendeshwa katika vituo vitatu; Hospitali ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo na katika Zahanati binafsi ya Chadibwa iliyoko Ukonga Mombasa, katika nyumba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu (IGP) Omar Mahita.

Awali majaribio hayo yalikuwa yamewalenga askari wa jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi, lakini wahusika hawakufanikiwa kuwashawishi na kuwapata, hivyo wakaamua kuwatafuta wananchi wa kawaida kuwafanyia majaribio hayo.





Waathirika hao walipata taarifa za majaribio hayo kutoka kwa baadhi ya askari Polisi na JWTZ ambao walikuwa ni madaktari, waliohusika kuwashawishi wananchi waathirika wa VVU.

Wengine kwa wahudumu katika hospital na vituo mbalimbali vya ushauri nasaha vya mashirika yasiyo ya Kiserikali wanaowahudumia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na Ukimwi, ikiwemo Pasada, ambako maafisa hao wa Polisi na JWTZ pia walikuwa wakienda kuwashawishi wajiunge.

Baada ya kupata taarifa hizo kila mmoja alitakiwa kuchagua kituo cha kwenda kufanyiwa majaribio hayo, yaani Zahanati ya Chadibwa, Ukonga au Hospitali ya Lugalo.

Huko walikuwa wakipewa maelezo ya majaribio ya dawa hiyo na wengine wakielezwa kuwa inatibu Ukimwi na kwamba imeshaonyesha mafanikio katika nchi mbalimbli. Aliyeridhia kushiriki alipewa fomu ya kujaza na kusaini kukubali kushiriki katika majaribio hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable