Homebongo habariBulaya adai mwekezaji Mchuchuma na Liganga hana mtaji Bulaya adai mwekezaji Mchuchuma na Liganga hana mtaji 0 ben June 15, 2021 Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya amesema utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga nchini Tanzania unasuasa kwa sababu mwekezaji hana mtaji. Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne Juni 15, 2021 wakati akiuliza swali la nyongeza.“Kuendelea na mradi wa Mchuchuma na Liganga kwenye Bunge letu bila utekelezaji ni aibu na mradi huo ni tangu Mary Nagu akiwa waziri (uwekezaji) mradi huu unasuasua kwa sababu mwekezaji hana mtaji ndio maana ameshindwa kulipa fidia,” amesema.Amehoji kwa nini Serikali inamkumbatia mwekezaji huyo badala ya kuachana naye na kutafuta njia nyingine akibainisha kuwa kama Rais Samia Suluhu Hassan anataka mradi huo uendelee kwa nini asitafutwe mwekezaji mwingine na Serikali ikawekeza vya kutosha.Akijibu swali hilo Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema ni kweli mradi huo umechukua muda mrefu na kubainisha kuwa mwekezaji huyo ana mkataba Shirika la Maendeleo nchini (NDC) ambao ni lazima uhitimishwe kisheria kwa sababu kwenda papara itasababisha matatizo.“Nimepata taarifa kuwa timu ya majadiliano ya Serikali leo inakaa. Tunaamini ndani ya mwezi huu mazungumzo yatakamilika, ama tuachane naye kisheria ama tutafute mwekezaji mwingine. Mradi huu lazima uanze mwaka ujao,” amesema. Tags bongo habari Newer Older