Virusi vya Corona: Serikali ya Tanzania yaonya kuhusu wimbi la tatu la Corona

Dk Leonard Subi ametoa maagizo kadhaa likiwemo la kuwataka wananchi kuvaa barakoa

CHANZO CHA PICHA,IPP MEDIA

Maelezo ya picha,

Dk Leonard Subi ametoa maagizo kadhaa likiwemo la kuwataka wananchi kuvaa barakoa

Serikali ya Tanzania imesema kuna viashiria vya wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 kutokana na virusi vya gonjwa huo kuingia nchini humo kutokea nchi jirani.

Mkurugenzi wa kinga wa Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi ametoa maagizo kadhaa likiwemo la kuwataka wananchi kuvaa barakoa. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi Juni 19, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)

"Wizara inawakumbusha wananchi wote kutopuuza ugonjwa wa Covid-19. Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huu katika nchi yetu." Mkurugenzi huyo ameukuliwa na gazeti la Mwananchi akiyasema hayo .

"Hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu zinazofanywa na wizara na mwingiliano kati ya watu wetu na mataifa mengine," amesema Dk Subi.

Dr Subi hakutoa takwimu za idadi ya raia wa Tanzania ambao wamepatikana na corona

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Dr Subi hakutoa takwimu za idadi ya raia wa Tanzania ambao wamepatikana na corona

Aliongeza kwamba idadi ya wagonjwa wanaopatikana na vizuri vya corona barani Afrika imeongezeka ndani ya wiki tano mfululizo zikiwemo nchi zinazopakana na Tanzania, "maambukizi yanaongezeka maradufu kuliko ilivyokuwa wimbi la pili." Gazeti hilo limemnukuu.

Katika maelezo yake amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono kutumia sabuni.

Dr Subi hatahivyo hakutoa takwimu za idadi ya raia wa Tanzania ambao wamepatikana na ugonjwa huo hadi kufikia sasa na haijajulikana Iwapo mamlaka zitatekeleza maagizo ya kuwazuia watu kukaribiana au kukusanyika .

Nchi jirani za Uganda na Kenya

Ilani hiyo ya serikali imejri wakati ambapo mataifa jirani ya Kenya na Uganda yamechukua hatua Zaidi kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.Siku ya Ijumaa rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza msururu wa masharti mapya ya kupambana na ongezeko la visa vya virusi vya Corona nchini humo.

Rais Museveni atangaza masharti zaidi kuzuia kusambaa kwa Corona

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Rais Museveni atangaza masharti zaidi (Lockdown)kuzuia kusambaa kwa Corona

Kwenye hotuba iliyopeperushwa kupitia runinga Ijumaa usiku, Museveni alitangaza kuwa usafiri wote wa kibinafsi na wa umma nchini umepigwa marufuku kwa siku 42 zijazo isipokuwa kwa huduma muhimu na mizigo.

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe na vivuko vingine vya mpaka wa ardhi hata hivyo vitabaki wazi kwa watalii na wale wanaorejea lakini mamlaka zimepewa jukumu la kuhakikisha kuwa hakuna kesi chanya au aina mpya za covid zinazoingia nchini humo.

Amri ya kutotoka nje imesongeshwa kutoka saa tatu usiku hadi saa moja usiku na itadumu hadi saa kumi na moja unusu alfajiri .Waendeshaji pikipiki, wanaojulikana kama Boda Boda wanaruhusiwa kubeba bidhaa tu.

Kazi zote zinazozingatiwa sio za lazima, shule na taasisi za kujifunzia, sehemu za ibada, na hafla za michezo pia zimefungwa kwa siku 42 zijazo.

Vituo vya biashara na maeneo ya biashara pia yamefungwa na wachuuzi wa soko wakiruhusiwa kulala kwenye vibanda vyao.

Masharti ya sasa ni sawa na ya mwezi Machi mwaka jana wakati nchi nzima ilipofungwa kabisa .

Museveni alisema hatua hizo ni muhimu kukomesha maambukizi ya sasa ya kijamii na kupeuka kuulemea kabisa mfumo wa utoaji wa huduma za afya.

Katika siku kumi na mbili zilizopita tu, nchi hiyo ilirekodi visa 15 800 na vifo 190 vinavotokana ana Corona .

Rais alionya kuwa kwa kiwango cha sasa cha maambukizo, mahitaji ya oksijeni katika vituo vya afya yangeongezeka mara 9 na nchi haiwezi kukabiliana na hali kama hiyo .

Rais pia ameamuru kwamba wahudumu wa baa na vilabu vya usiku ambao wanapatikana wakipuuza sheria za kufungwa wapokonywe leseni za kuhudumu

Baa na sehemu za burudani zilifungwa rasmi Machi 2020, lakini zingine zimekuwa zikifanya kazi kinyume cha sheria. Wale watakaopatikana wakihudumia wateja sasa watakamatwa na kutakiwa kulipa faini kubwa.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post