Watu 7 wamepoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea eneo la nane nane Morogoro ikihusisha magari matatu, Toyota Coaster lililogongana na Toyota Cresta T563 ASA na baadaye Coaster kugongana uso kwa uso na lori namba T658 DJZ.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Coaster ambaye alitaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.
Fortunatus Muslim na askari wengine wakiwa eneo la tukio
''Gari la abiria aina ya Toyota Costa lilitaka kulipita gari dogo aina ya Toyota Cresta ambapo gari hilo lilipoteza uelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Dangote na kusababisha vifo vya watu watano huku majeruhi wakikimbizwa hospitali kwa matibabu,'' - amesema Kamanda Muslim.
Magari yaliyohusika kwenye ajali
Naye mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando amezungumzia tukio hilo na kutoa rai kwa madereva kufuata kanuni na sheria za barabarani pia akiwaasa abiria kuchukua tahadhari hasa wanapoona mwenendo wa dereva hauridhishi ili kuepuka ajali kama hizo mbazo zinapotea nguvu kazi ya taifa huku mashuhuda wa tukio hilo wakielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea.