Vigogo wa soka wa nchini Misri , klabu ya Al Ahly waliifunga Kaizer Chiefs 3-0 katika mchezo ulichezwa kwenye dima la Mohamed V jijini Casablanca nchini Morocco Jumamosi usiku na kuwa timu ya Kwanza kuweka historia ya kutwaa taji hilo la ligi ya mabingwa wa Afrika kwa mara kumi.
Kutolewa nje kwa mchezaji wa Kaizer Chiefs Happy Mashiane aliyeonyeshwa kadi nyekundu kuliwafanya Al Ahly kupata goli la kuongoza kupitia mshambulijai Mohamed Sherif goli la pili la Wamisri hawa lilifungwa na Mohamed Kafsha katika dakika ya 74 ya mchezo kisha Amr Al Sulaya akafunga goli la mwisho.
Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane kombe hili linakuwa ni kombe lake la matatu la Ligi ya Mabingwa, Moja ya mafanikio yake ya kawaida, kwani ilikuja dhidi ya timu aliyoiunga mkono akiwa kijana, ilimfanya kuwa kocha wa pili tu wa Al Ahly kushinda taji la Afrika miaka miwili mfululizo, baada ya Manuel Jose wa Ureno mnamo 2005 na 2006.
Kabla ya mchezo huo, Mosimane alikuwa amedokeza kuwa atacheza mchezo huo kwa tahadhari kuwa na kujaribu kuwazuia kabisa Kaizer kitu ambacho kocha huyu Raia wa Afrika kusini alifanikiwa
Ahly imepata mataji 22 ya Afrika wakati Chiefs wana moja tu, Kombe la Washindi wa Kombe la Afrika la mnamo 2001, lakini baada ya kumaliza nafasi ya nane kwenye ligi, alama zingine 31 nyuma ya mabingwa Sundowns, kufikia fainali ilikuwa mafanikio makubwa sana.
Nyota wa Al Ahly El Shenawy na wenzake watano wa timu ya wanakwenda Tokyo kwenye mashindano ya Olimpiki kwenda kuiwakilisha timu yao ya taifa ya Misri.