Barcelona yamaliza mzozo na Neymar nje ya mahakama


 Timu ya Barcelona na mchezaji wake wa zamani Neymar wamefikia mapatano nje ya mahakama na hivyo kumaliza mzozo wao wa kisheria kwa "njia ya amani".

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, alidai kuwa Barca ilikataa kumlipa pauni milioni 37.2 za ruzuku ya baada ya kuhamia Paris St-Germain kwa malipo ya pauni milioni 200 mwaka 2017.

Barca walianza mchakato wa kisheria wa kutaka awarejeshee pauni milioni 8 alizopokea aliposaini mkataba mpya katika mwaka 2016.

Mwezi Juni mwaka jana, mahakama ya Uhispania iliamuru Neymar airudishie malipo ya pauni milioni 6.1 Barcelona.

Lakini taarifa zinasema kuwa alikuwa amekata rufaa dhidi ya uamuazi huo na kuanzisha kesi mpya, ambayo kwa sasa haipo.

Taarifa ya timu hiyo ya klabu ya La Liga imesema "FC Barcelona inatangaza kwamba imemaliza kesi ya mahakamani kwa mtindo wa amani kati yake na mchezaji wa Brazili Neymar.

"Kwa namna hiyo, mapatano ya malipo baina ya klabu na mchezaji yamekwisha sainiwa kumaliza kesi za kisheria zilizokuwa zikisubiliwa na pande mbili ‘’ , imesema taarifa hiyo.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post