Ghasia za Afrika Kusini: Ni nini kilicho nyuma ya ghasia na uporaji?

0

 

Looters take away few items left to grab in a vandalised mall in Vosloorus, on July 14, 2021

CHANZO CHA PICHA,AFP VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ghasia na uporaji viliibuka kutokana na kufungwa gerezani kwa Raiss wa zamani Jacob Zuma

Baadhi wanayaita matukio yaliyotokea wiki iliyopita ''kipindi cha giza'' cha Afrika kusini yenye demokrasia.

Lakini je ni zaidi ya kuibuka ghafla kwa hasira kulikosababishwa na kufungwa kwa rais wa zamani Jacob Zuma? Wachambuzi wengi wanasema ni kweli na kwamba kuna "msukumo wa tatu " wa huruma kwa rais huyo wa zamani unaohusika.

Lugha ya serikali pia imebadilika kwa kiasi kikubwa, kutoka kutosema mengi katika siku za mwanzo za ghasia hadi kutoa wito wa kile inachosema kimekuwa ni "uhujumu uchumi ".

Baadhi ya watoaji wa maoni wamekwenda hata mbali hadi kuonya kuwa ghasia zimekuwa na dalili ya "jaribio la mapinduzi" na "mwamko wa mageuzi dhidi ya serikali".

Rais Cyril Ramaphosa amesema kuwa ghasia zilikuwa zimepangwa awali, lakini hajasema ni nani alikuwa nyuma ya ghasia hizo .

Mhariri msaidizi Ferial Haffajee, wa gazeti la Daily Maverick, ameandika kuhusu mkakati ulioratibiwa wa ghasia, uliopangwa na washirika kumi na wawili wa rais wa zamani.

Akimaanisha vyanzo vya maafisa kadhaa kutoka ndani ya chama tawala cha African National Congress (ANC) na huduma za ujasusi , Haffajee ameainisha muundo wa mkakati huo- kuanzia uchomaji wa malori ya uchukuzi katika KwaZulu-Natal ulioshuhudiwa siku za mwanzoni mwa ghasia, hadi kufungwa kwa barabara muhimu inayotoka Durban hadi katika kitovu cha uchumi wa Afrika Kusini , Gauteng.

Maelezo ni kwamba hii ililenga kwa makusudi kudhoofisha zaidi uchumi ambao tayari ni dhaifu.

President Cyril Ramaphosa interacts with volunteers who embark on a clean up campaign on July 16, 2021

CHANZO CHA PICHA,AFP VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Rais Ramaphosa (Katikati) alitembelea mji wa Durban Ijumaa

Hii inaweza kuwa inatoka ndani ya chama tawala na huduma za taifa za ujasusi kwa pamoja.

Kuna nguvu mbili zinazopingana wazi katika ANC. Moja unaongozwa na Rais Ramaphosa, ambaye wafuasi wake wanasema taratibu anajenga upya taasisi za taifa baada ya muongo wa ufisadi na uporaji wakati wa utawala wa Zuma. Na mwingine kutoka kwa kikundi kinachofahamika RET , wanaomuonea huruma na wafuasi sugu wa rais wa zamani Jacob Zuma.

Huenda walinufaishwa na "kukamatwa kwa taifa " kwa Bw Zuma na wanahisi wametengwa na kasi ya kikundi cha Ramaphosa. Wanataka mabadiliko ya uongozi haraka na wana nufaika iwapo rais wa sasa amedhoofishwa.

Zuma alikuwa mkuu wa ujasusi maarufu sana wa ANC ndani na nje ya Afrika Kusini wakati wa enzi ya utawala wa Wazungu , kabla ya kupata ushindi mwaka 1990. Karibu miaka minne tangu aondoke madarakani, anaaminiwa kudumisha ushirika imara katika huduma za ujasusi nchini humo.

Hilo halishangazi. Wakati wa muhula wake madarakani kiasi kikubwa cha fedha kilielekezwa katika mwelekeo huo. Ukweli ni kwamba, kile kilichojitokeza katika tume ya uchunguzi wa ufisadi uliofanyika wakati wa urais wa Bw Zuma kinaonesha kwamba wakati wa miaka yake mamlakani, mifumo ya ujasusi iliundwa kando ya ile iliyokuwepo ikitekeleza matakwa ya rais.

Kama hilo ni kweli, mabaki ya miundo hiyo kweli bado yapo. Profesa Susan Booysen anasema kwamba licha ya ripoti ya mwaka 2018 kutambua "mifumo ya kando ya ujasusi" yenye uwezekano wa kuegemea au yenye huruma kwa rais wa zamani, ni machache yaliyofanywa na utawala wa sasa katika kuyang'oa makundi haya . Tunaweza kuwa tunashuhudia athari zake sasa.

Jacob Zuma speaks on the phone at the Randburg Magistrates Court on October 26, 2018, in Johannesburg

CHANZO CHA PICHA,AFP VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Madai ya ufisadi yalitawala wakati wa urais wa Zuma na kusababisha kujiuzulu kwake mwaka 2018

Washirika na wafuasi wa Zuma wanakana hili, wakisema kuhusisha makundi hayo na siasa katika mapambano au mifumo ya ujasusi ni jaribio la kuficha kushindwa vibaya kwa serikali katika utoaji wa huduma kwa masikini , pamoja na kubashiri na kushugulikia mlipuko wa ghasia.

Hakika jibu la serikali lilicheleweshwa na la ghafla - na lilikuwa kubwa kutokana na hilo.

Tangazo la ombi kwa ajili ya vikosi 25,000 vya ziada kwa miezi mitatu linapaswa kueleweka katika muktadha wa historia ya Afrika Afrika Kusini. Halikuwa la kawaida na ni kikosi kikubwa kuwahi kupelekwa kwenye maeneo ya Afrika Kusini tangu mwishoni mwa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Huku bado katika siku za kuelekea kutolewa kwa tangazo hili, uongozi wa kisiasa na kijeshi nchini humo ulisikika ukisitasita wazi kutumia wanajeshi zaidi - kando na kutangaza "hali ya dharura ya taifa ".

Hili halishangazi, kuona kile kinachotokea nchini humo.

Katika mkutano maafisa wa juu wa usalama, maafisa wa usalama waliwakumbusha watu wa Afrika Kusini kwamba wanajeshi hawako pale kutekeleza sheria, hiyo ni kazi ya polisi.

Hii ilikubalika katika utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini uliotangaza hali ya tahadhari katika miaka ya katikakati mwa -1980 wakati nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa sheria ya kijeshi.

Matumizi ya jeshi ni jambo linaloweza kuleta hisia za juu . Kwamba wamewapeleka wanajeshi kadhaa kwamba wameonyesha ukubwa wa hali.

Hii imeonesha wazi kwamba ni zaidi ya kudhibiti uporaji , na kuwa kitu fulani kilicho karibu zaidi na haja ya kulinda maisha na maslahi ya kimkakati ya taifa kama vile bandari ya Durban, hifadhi ya mafuta, mitandao ya mawasiliani na biashra muhimupamoja na mifumo ya usambazaji wa chakula na mafuta - vyote ambavyo vimetishiwa au kushambuliwa.

Kuna watu binafsi kadhaa ndani ya ANC na katika huduma za ujasusi za nchi wanaopoteza mengi iwapo kutakuwa na uwajibishwaji na utawala wa kisheria, kama ilivyotokea mapema mwezi huu wakati rais wa zamani alipofungwa na Mahakama ya katiba.

Kutokana na msukumo unaotokana na ukosefu wa usalama, kumekuwa na upungufu wa chakula na mafuta. Inaonekana dhahiri kwamba athari za ukosefu wa ajira ndizo zinazosababisha haya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable