Kawaida inatarajiwa watu maarufu na wenye majina makubwa katika jamii wawe nadhifu hasa kimwili, wakioenakana wenye kupendeza na kujipenda. Na hatua muhimu ya mtu kuwa nadhifu inaanzia kwenye kuoga ama kuosha mwili wako vizuri, kabla ya kufikiria kuhusu manukato, mafuta, nywele, viatu au mavazi.
Lakini si watu wote maarufu ni nadhifu wanaopenda kuoga ama kuosha miili yao, wako kadhaa ambao kuoga kwao ni hadithi ya mkizi ama jambo lisilo la maana na umuhimu. Wanaweza konekana nadhifu kwa macho kutokana na mavazi waliyovaa, ama mtindo wao wa nywele lakini wasiwe nadhifu wa mwili, wakawa na harufu isiyoendana na unadhifu wao wa nje.
Wapo waigizaji, wanamuziki, wanamitindo, wanamichezo na wanasiasa ambao wamewahi kukiri hadharani kwamba hawaogi kila siku kwa sababu kuoga kwao sio jambo lenye msingi sana na kutilia maanani wakati wote.
Majina kama Zac Efron, Julia Roberts, Shia Labeouf, Kristen Stewart, John Depp na Leonardo Dicaprio kuyaona kwenye orodha hii yanaweza kukushangaza, lakini kuoga kwa mtu hakuhusiani na anachokifanya, bali mazoea, tabia na namna anavyoona na kulichukulia suala hilo.
Wengine huoga kwa nafasi lakini sio lazima, kama hakuna nafasi amebanwa anaweza kukaa mpaka juma zima bila kuoga. Na unaweza kufikiria labda wanaweka akiba ya maji ama sabuni kumbe ni namna wanavyoamini na kulichukuliwa suala la kuoga. Wapo watu weng maarufu wenye Imani ndogo na kuoga miongoni mwao ni hawa wafuatao;
1: Brad Pitt
William Bradley Pitt ni muigizaji na mtayarishaji maarufu wa filamu duniani kutoka nchini Marekani, akimiliki kampuni kubwa ya utengenezaji wa filamu ya Plan B Entertainment.
Brad Pitt anatajwa kama miongoni mwa watu wenye ushawishi zaidi Marekani na kwa miaka mingi akitajwa na baadhi ya vyombo vya habari kama mwanaume anayevutia zaidi huku Maisha yake ya umaarufu yakimuweka juu na kuheshimiwa duniani kote.
Pamoja na sifa hizo, tuzo alizowahi kupata kama Golden Globe, Primetime Emmy na British Academy Film na uwezo wake wa kuongoza na kucheza filamu kwenye suala la kuoga kwake analiona la kawaida sana. 'Nina watoto sita, unachotakiwa kufanya ni kufuta sehemu muhimu tu za ndani na viungo. Najisaidia karibu siku nzima. Sina muda wa kuoga', alisema.
Muigizaji mwenzake kwenye filamu ya Inglourious Basterds, Eli Roth aliwahi kunukuliwa na mtandao wa People akisema kwamba baba huyo wa watoto sita amekuwa akiwapa ushauri matata wa namna ya kuwa msafi wakati wakiwa kwenye shughuli za kurekodi filamu zao. 'Alituambia kwamba ukiwa unatoka jasho na huna muda wa kuoga, chukua kitambaa chochote kidogo jifute kwenye makwapa na endelea na majukumu yako,' alisema Roth.
Roth mwenyewe anakiri kupokea ushauri huo wa Pitt na kuanza kutumia vitambaa hivyo hasa vile vya watoto laini kufanya makwapa yake yasitoe harufu wakati akiwa na shughuli nyingi na kukosa muda wa kuoga.
2: Mila Kunis
Milena Markovna Kunis si jina geni kwa wanaofuatilia sana filamu za kimarekani. Ni muigizaji na mtayarishaji. Uigizaji wake kwenye Black Swan ulimfanya kupata jina kubwa duniani na hata kupata tuzo ya Marcello Mastroianni kama muigizaji mchanga anayeibukia. Kwa waliongalia filamu ya The Boo of Eli, muigizaji aliyetumia jina la Solara basi ni Mila Kunis.
Pamoja na ukali wake kwenye filamu lakini kwenye suala la kuoga kuna ukakasi usiotoa majibu. Baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba hapendi kuoga mtangazaji wa kipindi maarufu cha Armchair Expert, Monica Padman alimuuliza Kunis nani kamfundisha kutokuoga akajibu," Wakati nakuwa hakukuwa na maji ya moto, kwa hiyo sikua naoga mara kwa mara'.
Kunis mwenye watoto wawili, Wyatt mwenye miaka 6 na Dimitri mwenye miaka 4 anaendelea kurithisha watoto kutopenda kuoga, kama ilivyo yeye hawaogeshi watoto wake mara kwa mara akirejea toka mwanzo kabisa wa uzazi wake 'Sikuwa yule mzazi anayeweza kuwaogesha watoto wake kila siku'.
Kwa sababu watoto hao angalau sasa ni wakubwa, Kunis anasema ameweka utaratibu maalumu , 'Ukiona watoto wamechafuka , ndo unawaogesha, alisema ' inginevyo, hakuna maana ya kufanya hivyo'.
3: Ashton Kutcher
Christopher Ashton Kutcher muigizaji, mwanamitindo, mtayarishaji wa filamu na mjasiriamali aliyewekeza kwenye makampuni zaidi ya 60 duniani miongoni mwa makampuni yenye hisa zake nyingi ni Skype Foursquare, Airbnb, Path na Fab.com na kumuingizia utajiri mkubwa unaokadiriwa kufikia dola $220milioni.
Tamthilia ya 70's iliyoanza mwaka 1998 mpaka 2006 inayotajwa kutazamwa na watu wengi zaidi, Kutcher alikua kinara wake lakini akang'ara vizuri na filamu za Dude where's my Car?, Guess who 2005 na Butterfly Effects.
Kutcher ni mume wa Muigizaji Mila Kunis, Kama ilivyo kwa mkewe na yeye anasema haoni kama kuna umuhimu sana wa kuwa unaoga kila siku. Alionyesha wazi kwamba nay eye si mtu wa upenda kuoga alipohojiwa kwenye Podcast ya Armchair expert kinachoongozwa na watangazaji wawili Dax Shepard na Monica Poadman.
Kutcher alisema kila siku anachokifanya ni kuosha tu sehemu za mwili wake anazodhani zikiachwa zinaleta harufu 'Naosha 'makwapa, sehemu za siri na chini ya mapaja si zaidi ya hapo', alisema na kuongeza kwamba ana kawaida ya 'kupitisha maji kidogo kwenye uso wangu baada ya kutoka mazoezini kuondoa jasho na chumvichumi usoni'.
Kwa kauli ya Kutcher, inamaanisha familia yao na mkewe Kunis, yenye watoto wadogo wawili; Wyatt na Dimitri haiamini kuhusu kuoga. Unaweza kujiuliza watoto wakuwa kwenye hali gani?
4: Robert Pattinson
Robert Douglas Thomas Pattinson ni muigizaji Muingereza, akitajwa na jarida la TIME kama mmoja wa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani akiingia pia kwenye orodha ya Forbes ya watu maarufu 100 duniani.
Filamu za Twilight, Bravo Otto na The King zimemtambulisha kama muigizaji mkubwa kwa uwezo aliouonesha na amecheza kama Cedric Diggory kwenye filamu ya Harry Potter.
Filamu hizi zimemuweka juu kiasi kwamba ukitaja waigizaji watano wanaolipwa pesa nyingi kwa sasa duniani, jina la Pattinson huwezi ukaliweka kando. Utajiri Pattinson unakadiriwa kufikia dola $100million.
Pamoja na hayo kwenye suala la kuoga, Pattinson anatazama kwa jicho tofauti kabisa na kujikuta kuwa kwenye orodha ya miongoni mwa watu maarufu wasiojali kuhusu kuoga.
Nyota wa Twilight alipoulizwa katika mahojiano yake na kituo cha Extra TV, kuhusu tetesi kwamba aliwahi kukaa wiki sita bila kutia maji nywele zake, Pattinson alikiri na kujibu 'Inawezekana. Siju, sioni sana maana ya kuosha nywele. Na kuongeza 'Sioni kabisa maana ya kuoga au kuosha nywele kila siku, kama hujali kwamba nywele zako ni safi ama sio safi, kwanini uzioshe?
Pamoja na kukiri kwake kuhusu suala la kuosha nywele asivyoliona la maana, maneno ya Pattinson yaliashiria kwamba hajali kuhusu kuoga mwili mzima na kuoga si suala linalomsumbua kichwani.
Miaka mitatu kabla ya mahojiano yake na Extra, mmoja wa watu wa karibu waliowahi kufanya kazi pamoja kwenye filamu ya Twilight aliiambia MTV kwamba walikuwa na hofu na usafi wa Pattinson. 'Ananuka, yani harufu mbaya, nadhani haogi na inawafanya watu wanaofanya nae kazi wakati wa kutengeneza filamu kupata tabu', alisema.
5: Naya Rivera
Naya Marie Rivera ni muigizaji wa marekani, muimbaji na mwanamitindo. Unaijua tamthilia ya Glee, Naya aliigiza vyema. Alipata tuzo nyingi zikiwemo mbili za Grammy, SAG, ALMA na akaorodheshwa kuwania tuzo ya Brit.
Ni Miongoni mwa warembo na waigizaji wenye mvuto na muonekano mzuri, lakini si mpenda kuoga kama ambavyo ungefikiria. Alifariki Julai 8 mwaka 2020 lakini wakati wa uhai wake aliwahi kunukuliwa kwenye televisheni ya taifa kupitia The View akisema kwamba huwa haogi kila siku, anaoga mara moja moja tu pale inapobidi.
'Nina mtazamo wangu kuhusu kuoga, ambao ni kwamba, nafikiri watu weupe wanaoga sana na mara nyingi kulikowatu wengine. Nadhani kwamba, kuoga zaidi ya mara moja au kila siku ni jambo la watu weupe', alisema Rivera akinukuliwa na mtandao wa lifeandstylemag.
Pamoja na kwamba hakuwa anapenda kuoaga, alifariki kwa kuzama maji kwenye ziwa Piru Julai 8, 2020 alipokwenda kuogelea yeye na mtoto wake wakati huo mtoto huyo alikuwa na miaka minne. Mwili wake uliokotwa siku tano baadae na kuzikwa.