Kukamatwa kwa kiongozi wa vuguvugu la kujitenga Nnamdi Kanu, kumesababisha pigo kubwa kwa kundi lake, na pengine kuwa mwisho wa harakati zake.
Kiongozi wa kundi hilo la Indigenous People of Biafra (Ipob), kundi linalotaka kujitenga kwa jimbo la kusini -mashariki mwa Nigeria bado ameendelea kuwa shujaa kwa maelfu ya wafuasi wake.
Kwa zaidi ya muongo mmoja, matangazo yake ya redio ya moto na machapisho ya mitandao ya kijamii yalikuwa miiba kwa serikali ya Nigeria lakini mabadiliko yake kuwa vita vya silaha mnamo 2020 ilionekana kama hatua ya mbali sana.
Kundi la Ipob lenye silaha-Mtandao wa ulinzi wa Mashariki-umekuwa ukishutumiwa kuua watu takribani 60 katika miezi ya karibuni, wengi wao maafisa wa polisi, ingawa kundi hilo limekana madai hayo.
Kukamatwa kwa Bw. Kanu siku ya Jumapili iliyopita kunaonekana ni tukio la mwisho kufanywa na serikali iliyoazimia kutuliza ghasia.
Picha za kukamatwa kwake, zaidi ya kitu kingine chochote, zingeweza kudhoofisha imani ya hata wafuasi wake wenye nguvu.
Haikuwa mara ya kwanza kwa Nnamdi Kanu mwenye miaka 53 kufungwa pingu, lakini tofauti na hapo awali uasi wake wa kimila haukuwepo.
Bwana Kanu ilisemekana aliligeuza shirika hilo kuwa la mtu mmoja, akiwatenga wafuasi wake waaminifu zaidi, na kwa hivyo sasa kuna ombwe la uongozi.
''Migogoro inayohusu masualaya fedha na shutuma kwamba hakuwasiliana na wadau muhimu juu ya kuundwa kwa mrengo wenye silaha hayakuwaridhisha wengi," alisema Chiagozie Nwonwu wa BBC Igbo, ambaye alizungumza na Bw Kanu mnamo 2019 akiwa uhamishoni.
Mmoja wa wale waliogombana na Bw Kanu na kuacha shirika mwaka jana alikuwa naibu wake wa zamani, Uche Mefor, mwanachama anayeheshimiwa wa kikundi hicho ambaye alichukua nafasi wakati kiongozi huyo alipokuwa kizuizini hapo awali.
Madai ya matumizi mabaya ya fedha zilizochangwa pia yamesababisha kuondoka kwa wafuasi waaminifu nchini Marekani na Uingereza.
Mahali hapa, uti wa mgongo wa vuguvugu pia umeondoka, kwani wafuasi waliokuwa na uzoefu katika mapambano hayo wameuawa au kukamatwa na vikosi vya usalama vya Nigeria.
Hisia za muda mrefu kuhusu kutengwa
Waigbo wengi wanahisi kutengwa katika siasa za Nigeria
Kabila la tatu kwa ukubwa nchini Nigeria, bado hawajatoa rais tangu miaka ya 1960 na kushutumu serikali kupuuza eneo lao.
Hisia hizi zimeongezeka tangu Rais Muhammadu Buhari aingie madarakani mnamo 2015, na mazungumzo yake hayajasaidia.
Hivi karibuni alirejelea vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati akiapa kupambana na Ipob, na kusababisha Twitter kufuta tweet yake, na zamani alisema wale waliompa 5% ya kura [kama vile kusini-mashariki] wasitarajie kutendewa sawa na wale ambao waliompatia 95%.
Maoni kama hayo yalisaidia kumshawishi Bw Kanu, mtu mashuhuri licha ya matangazo yake ya redio, kujulikana.
Rais mwingine yeyote angeweza kumpuuza lakini sio Bw Buhari, jenerali wa zamani wa kijeshi.
Bwana Kanu alikamatwa mnamo 2015 aliporudi Nigeria lakini hii ilimuongezea umaarufu.
Mwanamume ambaye alifukuzwa kama na watu wengi wa Nigeria, hata ndani ya kabila lake, alikuwa mtu wa kabila la Igbo anayezungumzwa zaidi.
Wale wanaomjua wanasema ilikuwa ni hali aliyokuwa akitamani na mara moja aliachiliwa kwa dhamana mnamo 2017 hakuangalia nyuma tena.
Kutoroka kwa namna ya ajabu
Aliunda Huduma za Usalama za Biafra (BSS), wanamgambo ambao walivaa mavazi meusi na kufanya gwaride katika mji wa mashariki wa Abia, jimbo la nyumbani kwake.
Alimshutumu rais kwa kuweka mipango ya kuifanya Nigeria kuwa taifa la Kiislamu.
Bw Buhari alihisi ameona vya kutosha na baada ya mahakama kulisema Ipob kama shirika la kigaidi, jeshi liliingia, likafanya shambulio nyumbani kwa Bw Kanu mnamo Septemba 2017.
Alitoroka kwa namna ya ajabu
Wengi walidhani huo ndio mwisho, lakini aliibuka tena Ulaya mnamo 2018 na matangazo ya redio yakaanza tena, wakati huu yakiwashikilia mgogoro wa wafugaji wa Nigeria ili kuchochea mivutano ya kikabila nchini humo.
Mwaka jana, yalifanyika maandamano ya #EndSars dhidi ya ukatili wa polisi lakini wengi wanaamini huu ndio mwanzo wa kuanguka kwake.
Wakati majambazi walipoteka maandamano hayo kote Nigeria, Bw Kanu aliwaamuru wafuasi wake kushambulia vituo vya polisi.
Kwa mtu ambaye alikuwa wazi dhidi ya mapigano ya silaha katika siku za mwanzo za Ipob, ni ngumu kujua ni nini kilibadilika.
Watu wengi wanashuku kuwa shambulio la 2017 dhidi ya nyumba yake na vifo vya washirika vilichochea uamuzi wake wa kukipa kikundi hicho silaha.
Mwisho wa 2020 aliifufua BSS na kuipa jina tena Mtandao wa Usalama wa Mashariki (ESN).
Wakati BSS ilikuwa wanamgambo , ESN ilikuwa karibu na mpango halisi.
Wanachama, wakiwa wamevaa mavazi meusi na kofia nyekundu, walifundishwa katika misitu ya kusini-mashariki, kulikuwa na mlolongo wa uongozi na muhimu zaidi walikuwa na bunduki za AK-47 zilizoibiwa kutoka vituo vya polisi.
Kati ya Septemba 2020 na Mei 2021, kulikuwa na wimbi la mashambulio kwenye vituo vya polisi na vituo vingine vya umma kusini-mashariki ambayo mamlaka ililaumu kundi la Ipob.
Kwa watu wengi, haswa vijana wenye huruma kwa sababu ya Ipob, operesheni ya jeshi ilifungua macho juu ya jinsi vita ilivyokuwa.
Biashara zilifungwa, amri za kutotoka nje ziliwekwa na watu walitembea mikono yao juu ya vichwa vyao walipofika kwenye vituo vya ukaguzi vya jeshi.
Kwa wakati huu, hisia zilianza kugeuka dhidi ya Ipob na kiongozi wake na kwa kukamatwa kwake, anajiunga na watu wa vuguvugu hilo wengine wa Igbo.