Kutoka kuwa hafai hadi kuwa shujaa: Mfahamu mkufunzi wa timu ya England Gareth Southgate

 

Photo collage showing Southgate as a player and a manager

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Akiwa mchezaji, Gareth Southgate alikosa kufunga penati iliyoiandoa Uingereza katika michuano ya Euro mwaka 1996, lakini chini ya ukufunzi wake amefanikiwa kuifikisha timu yake katika fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza

Timu ya kandanda nchini England ni maalum sana: Hawajashinda mashindano makubwa tangu waliposhinda Kombe la Dunia miaka 55 iliyopita.

Hii huenda ikabadilika Jumapili hii, wakati England itakaposhuka dimbani na Italia katika fainali ya kombe la Euro 2020 mjini London.

Kocha Gareth Southgate amekuwa sehemu kubwa ya safari hiyo iliyojumuisha hadithi ya ukombozi wa kibinafsi kwake.

Mwanzo uliopingwa

Wakati Gareth Southgate alipoteuliwa kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya kandanda ya Uingereza mwezi Novemba mwaka 2016, alikuwa na masuala makuu mawili ya kushughulikia.

Kwanza Southgate hakuwa na rekodi iliyothibitishwa.

Kazi hiyo ambayo inaangaziwa na waandishi wa habari na kuchunguzwa kuliko anavyochunguzwa Waziri Mkuu, moja kwa moja ilimweka katika kibarua kigumu kuanzia mwanzo.

Uingereza haijawahi kushinda taji lolote kuu la kandanda tangu mwaka 1966 iliposhinda kombe la dunia

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Uingereza haijawahi kushinda taji lolote kuu la kandanda tangu mwaka 1966 iliposhinda kombe la dunia

Suala la pili ni kumbukumbu ya zama zake akiwa mchezaji: alikosa kufunga penati iliyoiandoa Uingereza katika michuano ya Euro mwaka 1996 Uingereza ilipokutana na Ujerumani katika uwaja wa Wembley uliojaa mashabiki.

Aliwahi kukataa ofa ya kwanza ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya England miezi kadhaa ya awali kwa kuhofia kukataliwa na mashabiki na kukosolewa na vyombo vya habari.

Miaka mitano baadaye , Southgate -na England sasa wana nafasi ya kuondoa mkosi wa kushindwa katika fainali watakapomenyana na Italia, katika mechi itakayochezwa uwanja wa Wembley, ambako kulichezwa mechi ya fainali ya kusisimua miaka 25 iliyopita.

'Je anatosha?'

Italia mabingwa mara nne wa Kombe la Dunia, ilishinda kombe la Euro mwka 1980 na hawajashindwa katika mechi 33, rekodi ambayo ni ndefu zaidi katika historia ya mpira wa miguu. Hawajapoteza mechi tangu Septemba 2018.

Uingereza haijawahi kushinda taji kuu la kandanda barani Ulaya.

Katika mashindani ya kimataifa, Southgate aliye na umri wa miaka 50 amewashinda watangulizi wake na hata rekodi ya meneja Alf Ramsey aliyeshinda Kombe la Dunia.

Hii ni ishara nzuri kwa kocha huyo ambaye uteuzi wake ulipokelewa kwa hisia mseto huku baadhi ya vyombo vya habari vikihoji uwezo wake kupitia vichwa vya habari vya kukejeli kama ile ya ''Je anatosha?'' iliyoandikwa na BBC Michezo?"

Gareth Southgate celebrates England's win against Denmark in the Euro 2020 semifinals

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Uteuzi wa Southgate kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ungereza awali ulipingwa lakini amefanya vyema kuliko watangulizi wake

Kikwazo kingine kilichomkabili ni kwamba alikuwa mpole na mwanamume mwenye haya kutoka Watford, kaskazini mwa London, lakini ilibidi atafute mbinu ya kukabiliana hali hiyo.

Akiwa na miaka 16, wakati huo akichezea katika timu ya chipukizi ya Crystal Palac, kocha Alan Smith alipendekeza kinda Gareth anahitaji "kujiimaisha" kuwa mwanasoka hodari au aamue kuwa ajenti wa masuala ya usafiri.

Lakini aliendelea mbele na kucheza mechi 503 akiwa na Palace, Aston Villa na Middlesbrough na pia kuiwakilisha England katika mechi 57.

Kushindwa na uvumilivu

Hatua ya kupoteza penalti muhimu dhidi ya Ujerumani mwaka 1996 ilimuathiri sana na yeye mwenyewe amekiri bado anajutia kukosa penalti hiyo.

"Huenda ulikuwa unacheza mechi kubwa ambayo timu yako imewahi kucheza ndani ya miaka 30 wakati huo alafu unatoka uwanjani ukihisi umechangia kuondolewa kwa timu yako mashindano," alisema mwaka jana.

"Kwa kiwango kidogo bado nahisi, nilipoteza penalti hiyo kutokana na presha ya mashabiki na hofu ya kushindwa kufikia matarajio yao ni hali ambayo huwaathiri sana wachezaji.''

Southgate aliiwakilisha nchi yake kwa miaka minane baada ya kukosa penati hiyo muhimu mwaka 1996

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Southgate aliiwakilisha nchi yake kwa miaka minane baada ya kukosa penati hiyo muhimu mwaka 1996

Hatua yake ya kuendelea kucheza katika timu ya taifa ya England baada ya kisa hicho ni dhihirisho la uvumilivu wake kama mchezaji.

Alipochukua usukani wa kuwa kocha wa timu ya taifa hakuchukua muda kuwathibitishia uweledi wake kwa wale waliomtilia shaka.

Katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2018 huko Urusi, timu ya taifa ya Uingereza ilifika nusu fainali ya mashindano hayo kwa mara ya tatu katika historia yake.

Kuunga mkono kikamilifu 'kupiga goti'

Hata hivyo hii haimaanishi wakosoaji wake walikoma kumuangazia. Vyombo vya habari na wachezaji wenzake wa zamani walimchukulia kuwa ''mwangalifu sana ''.

Hashtag ya #southgateout kumtaka aondolewe ilipata umaarufu kwenye Twitter siku ya mechi ya kwanza ya England katika michuano ya Euro 2020.

Southgate pia alikosolewa kwa kuunga mkono uamuzi wa wachezaji wake "kupiga goti" kabla ya mchezo mwaka jana kupinga ubaguzi wa rangi.

Ilikuwa ni hali isiyokuwa ya kawaida katika historia ya timu ya taifa ambayo imekuwa ikilalamikiwa mara kwa mara na baadhi ya mashabiki wa England kwenye mechi.

England players kneeling down ahead of the game against Denmark

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Hatua ya wachezaji wa England "kupiga goti" ksbls y smechi imekosolewa na baadhi ya mashabiki

Chini ya ukufunzi wa Southgate, Ungereza ina moja ya kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji wadogo katika historia yake, nusu ya wachezaji hao wakiwa na wazazi au mababu waliozaliwa nje ya nchi hiyo.

Kocha huyo hakujali kuzomewa bali aliunga mkono hadharani haki ya wachezaji kuhamasisha jamii kuhusu masuala yasiyohusiana na michezo.

"Siamini kwamba tunastahili kuangazia mchezo wa kandanda pekee," Southgate alisema katika barua ya wazi iliyochapishwa katika tovuti ya wachezaji ya Tribune.

"Nina jukumu katika jamii kutumia sauti yangu kuangazia masuala yanayotuhusu, pia wachezaji wana haki sawa hiyo."

Shabiki nje ya uwanja wa Wembley akiwa na bango la meneja wa England Gareth Southgate

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Southgate aliwahi kukataa uteuzi wa kuwa kocha wa timu ya taifa kwa kuhofia hatapokelewa vyema - hilo halionekani kuwa kikwazo tena

"Ni jukumu lao kuendelea kushirikiana na umma kuangazia masuala kama vile usawa, ujumuishwaji na ubaguzi wa rangi."

Lakini kocha huyo anafahamu fikra kwamba cha msingi ni utenda kazi wa timu uwanjani: nchi inatazamia "kurejea nyumbani" kwa taji la soka.

Je atakuwa Sir Gareth?

"Najivunia sana wachezaji wangu," kocha huyo alisema baada ya ushindi wa Jumatano dhidi ya Denmark katika michuano ya nusu fainali ya Euro 2020.

"Lakini bado tuna kibarua kigumu kinachotusubiri na ambacho tunaamini tutashida.

Uingereza ikiishinda Italia siku ya Jumapili katika uwanja wa Wembley, Southgate atamaliza ukame wa mataji maarufu ya mchezo huo, na huenda akapiga goti yeye mwenyewe - mbele ya Malkia Elizabeth II.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post