Moto waibuka katika ibada ya mazishi ya Mchungaji TB Joshua



Moto umewaka usiku wa Jumatatu katika ghala lililopo ndani ya kanisa la mhubiri aliyekuwa na ushawishi mkubwa nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos.

Moto huo ulitokea wakati wa mchakato wa mazishi yake ulioanza jana kwa kuwashwa mishumaa kwa ajili ya kumuenzi Nabii TB Joshua aliyefariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 57.

Moto uliwaka wakati wa ibada ya iliyokuwa sehemu ya mazishi ya TB Joushua iliyoongozwa na mjane wake Everlyne Joshua
Image caption: Moto uliwaka wakati wa ibada ya iliyokuwa sehemu ya mazishi ya TB Joushua iliyoongozwa na mjane wake Everlyne Joshua

Waombolezaji na waumini waliokusanyika katika kanisa lake la Synagogue Church of All Nations kwa ibada ambayo iliongozwa na mjane wa TB Joshua Evelyn Joshua walikanyagana walipokuwa wakitimua mbio kuokoa maisha yao.

Kanisa hilo limesema moto huo ulitokana na hitilafu ndogo ya umeme. Limesema moto huo umezimwa na hapakuwa na mtu yeyote aliyeathiriwa na moto huo.

LAGOS STATE GOVERNMENT
Image caption: Kamishna wa jimbo la Lagos wa masuala ya afya Prof. Akin Abayom akisaini kitabu cha mazishi ya TB Jumatatu usiku

TB Joshua atazikwa katika eneo la kanisa hilo Ijumaa.

Unaweza pia kusoma:

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post