Ollie Bibby: Hospitali yaomba msamaha kwa kumuzia mama asimuone mwanae aliyekuwa anakufa

 

Ollie and Penny

CHANZO CHA PICHA,BIBBY FAMILY

Maelezo ya picha,

Ollie alikuwa anajitolea sana ikiwemo kusaidia watu wasio na makazi wanaoshi mtaani hasa karibu na Hospitali alikolazwa kwa kuwapa mavazi, alisema maa yake, Penny

Hospitali moja nchini Uingereza imelazimika kuomba msamaha na kuhaidi kurekebisha utaratibu wa watu kuwatembelea wagonjwa baada ya kuwakataza wazazi wa familia moja kumtembelea mtoto wao aliyekuwa katika siku za mwisho za uhai wake.

Ollie Bibby, mkazi wa Benfleet Kusini, Essex, alifariki dunia Mei 5 mwaka huu kwa ugonjwa wa Leukaemia katika hospitali ya chuo Kikuu kishiriki cha London.

Kutokana na kugusa wengi, Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer, aligusia suala hilo bungeni.

Mama yake na Bibby, Penny alisema: "unachota tu kutokana na tukio hili, ni kurekebishwa kwa sera. Hili lazima likome."

Mama huyo alisema barua liyoipata kutoka kwa kiongozi wa Hospitali hiyo, Tim Jaggard, ilikuwa yenye ujumbe ambao hakuutarajia na wa kushangaza akiamini inaweza uwa msaada kwa watu wengine walio na wapendwa wao Mahspitalini.

"Haya ndiyo tuliyokuwa tunataka, hatutaki familia zingine zipitie tuliyoyapitia sie. Tuna hisi Ollie angefarijika kuwa naye pamoja naye kando kwenye safari ya umauti," alisema.

Ollie

CHANZO CHA PICHA,PENNY BIBBY

Maelezo ya picha,

Ollie alikuwa mtu wa watu na mwenye marafiki wengi akipenda sana mchezo wa mpira wa miguu. Hiyo ni kwa mujibu wa familia yake.

Alisema Bwana Jaggard aliandika akisema kwamba Hospital inajaribu kuweka uwiano wa usalama wa wagonjwa na huruma ya kuwatembelea, na kukiri kwamba walikosea na kuomba msamaha.

Barua hiyo iliongeza "Tunataka kukuhakikishia kwmaba tunaangaia utaratibu namna gani tunatekeleza maelekezo na muongozo wa kitaifa."

Bibby anasema sio sahih sheria ya kutembelea wagonjwa inafanya kitu cha bahati nasibu, kwamba kila hospitali inatafsiri kivyake miongozi ya kitaifa.

'Tulifanywa kama wahalifu'

Mtoto wake alikuwa na miaka 26, alifariki siku moja kabla ya Waziri wa afya nchini humo, Matt Hancock hajapigw apicha akimbusu mmoja wa wafanyakazi wa ofisi yake, na kupelekea kujiuzulu kwa kiongozi huyo.

Bibby aasema alinyimwa kumuangalia mtoto wake kwa kisingizio cha kufuata sharti la umbali kwa sababu ya janga la corona. Anasema si sawa kwa wagonjwa wanaohitaji faraja ya ndugu. Kuhusu mwanae anasema alikuwa kama mfungwa katika hospitali hiyo, baada ya wazazi kunyimwa kumtembelea. Pamoja na kubembeleza sana uongozi wa Hospitali angalau awe karika wakati huo mwanae akihitaji faraja, aligonga mwamba. Tulifanyw akama wahalifu kwa sababu ya masharti ya Covid 19.

Bungeni, Sir Keir akauliza swali kuhusu hilo kwa waziri mkuu, baada ya waziri mwenye dhaman Hancock kujiuzulu. Bibby alisema anahisi waziri mkuu Boris Johnson, aliliweka kando na anahisi ailikwepa.

Simon and Penny Bibby
Maelezo ya picha,

Wazazi wa Ollie, Simon na Penny walikuwa na hasira wakati waziri Matt Hancock alipovunja masharti ya kukaa mbali , wakati wao wakinyimwa kumuona mtoto wao aliyekuwa hoi hospitali.

Ollie and Georgie

CHANZO CHA PICHA,PENNY BIBBY

Maelezo ya picha,

Mpenzi wa Ollie, Georgia ndiye pekee aliyeruhusiwa kumuona mara mbili katika wiki saba alizolazwa Hospitali kabla hajafariki

Katika taarifa yake, Msemaji wa Hopsitali ya UCLH alisema mara zote Hospitali hiyo inafuata taratibu zilizopo za kitaifa na miongozo yake ili kuwalinda wagonjwa ambao wako kwenye hatari ya kupata maambukizi ya corona. Kwa mantiki hii, mtoto wa Bibby, Ollie alikuw amiongoni mwa wagonjwa waliopaswa kulindwa kwa kutotembelewa.

"Imekuwa nguvu kuweka uwiano wa kulinda wagonjwa na huruma ya watu kuwaona wakati huu wa janga la corona, lakini tunaamini watumishi wetu watafanya wanachokiweza ili kuboresha hilo', ilisema sehemu ya taarifa ya msemaji huyo na kuogeza 'Tunawasiliana na familia ya Oliver angalau kujua na kujifunza waliopita, na tunaomba radhi sana kwa wazazi wake, kaka zake, familia nzimana marafiki katika kipindi hiki kigumu kwao."

Ollie and family

CHANZO CHA PICHA,PENNY BIBBY

Maelezo ya picha,

Ollie alikuw akaribu sana na familia yake, wakiweka kaka zake watatu Sam, Casey na Ronnie

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post