Anayatumia majina matatu - Park Jin-hyok, Pak Jin-hek na Park Kwang-jin.Lakini hakuna hakikisho kwamba yote ni majina yake halisi kwa hivyo usiyaamini .
Mwaka wa 2016 wadukuzi wa Korea Kaskazini walipanga wizi wa $ 1bn kwenye benki ya kitaifa ya Bangladeshi na nusura watoroke na fedha hizo . Hata hivyo walifaulu kukwepa na dola milioni 81 .
Kikosi cha wadukuzi wanaoungwa mkono na Korea Kaskazini kina mwanamme mmoja ambaye anatumia majina mbali mbali.Yeye ni miongoni mwa washukiwa wakuu na kwa wengi anafahamika kama Park Jin-hyok
Katika tasnia ya usalama wa kimtandao, wadukuzi wa Korea Kaskazini wanajulikana kama Kikundi cha Lazaro, kumbukumbu ya mtu katika bibilia ambaye alirudi kutoka kwa wafu; wataalam walioshughulikia virusi vya kompyuta vya kikundi hicho waligundua kwamba virusi walivyotengeza vilikuwa sugu .
Mengi hayajulikani kuhusu kikundi hicho, ingawa FBI imetoa mchoro wa picha ya mtu anayeaminika kuwa mtuhumiwa mkuu: Park Jin-hyok, ambaye pia anayatumia majina Pak Jin-hek na Park Kwang-jin.
Inamuelezea kama muunda programu wa kompyuta aliyehitimu kutoka moja ya vyuo vikuu vya juu nchini na kwenda kufanya kazi katika kampuni ya Korea Kaskazini, Chosun Expo, katika mji wa bandari wa China wa Dalian, akiunda programu za michezo ya kubahatisha na kamari kwa wateja ulimwenguni kote.
Alipokuwa Dalian, alianzisha anwani ya barua pepe, akaunda wasifu , na akatumia mitandao ya kijamii kujenga mtandao wa mawasiliano.
Nyayo za mtandao zilimweka Dalian mapema mwaka 2002 na kuendelea hadi 2013 au 2014, wakati shughuli zake za mtandao zinaonekana kutoka mji mkuu wa Korea Kaskazini, Pyongyang, kulingana na hati ya kiapo ya mchunguzi wa FBI.
Shirika hilo limetoa picha iliyochomolewa kutoka barua pepe ya 2011 iliyotumwa na meneja wa Chosun Expo anayemtambulisha Park kwa mteja wa nje.
Inaonyesha mwanamume Mkorea aliyenyolewa kwa njia safi aliye na miaka 20 au 30, amevaa shati nyeusi iliyopigwa pini na suti ya rangi ya chokoleti. Hakuna kitu cha kawaida, kwa mtazamo wa juu, mbali na sura iliyofifia kwenye uso wake.
Ni njama waliopanga kwa miaka na nusura wadukuzi wa Korea Kaskazini waibe dola bilioni moja
Lakini FBI inasema kwamba wakati alikuwa akifanya kazi kama muunda programu wakati wa mchana, alikuwa mdukuzi sugu wakati wa usiku.
Mnamo Juni 2018, mamlaka ya Marekani ilimshtaki Park kwa shtaka moja la kula njama na utumiaji mbaya wa kompyuta, na moja ya kula njama ya kufanya ulaghai wa Kielektroniki (ulaghai unaojumuisha barua, au mawasiliano ya elektroniki) kati ya Septemba 2014 na Agosti 2017.
Anakabiliwa na hadi 20 miaka gerezani ikiwa atakamatwa. (Alirudi kutoka Uchina kwenda Korea Kaskazini miaka minne kabla ya mashtaka kufunguliwa.)
Lakini Park, ikiwa hilo ndilo jina lake halisi, hakuja kuwa mdukuzi wa serikali mara moja. Yeye ni mmoja wa maelfu ya vijana wa Korea Kaskazini ambao wamefunzwa tangu utotoni kuwa magwiji wa kimtandao - wanahisabati wenye talanta wenye umri wa miaka 12 waliochukuliwa kutoka shule zao na kupelekwa kwa mji mkuu, ambapo wanapewa masomo makali kutoka asubuhi hadi usiku.
Yaonekana Korea Kaskazini imetoa baadhi ya wadukuzi wenye nguvu sana na wa hali ya juu, bila hata ulimwengu kufikiria hilo lingewezekana .
Kuelewa kwanini, Korea Kaskazini imeweza kukuza vitengo vya wasomi wa vita vya kimtandao inahitaji kuangalia familia ambayo imetawala Korea Kaskazini tangu kuanzishwa kwake kama taifa la kisasa mnamo 1948: Familia ya Kim.
Mwanzilishi Kim Il-sung aliunda taifa linalojulikana rasmi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea kwa mfumo wa kisiasa ambao ni wa kijamaa lakini unafanya kazi zaidi kama kifalme.
Mwanawe, Kim Jong-il, alitegemea jeshi kama msingi wake wa nguvu, akiichokoza Marekani kwa majaribio ya makombora la balistiki na vifaa vya nyuklia.
Ili kufadhili mpango huo, serikali iligeukia njia haramu, kulingana na mamlaka ya Marekani- pamoja na uundaji wa sarafu za dollar zenye ubora wa juu kwa Superdollars ambazo zilikuwa bandia lakini zenye ubora mkubwa .
Kim Jong-il pia aliamua mapema kuingiza mtandao katika mkakati wa nchi hiyo, kuanzisha Kituo cha Kompyuta cha Korea mnamo 1990. Inasalia kuwa nguzo muhimu ya shughuli za IT za nchi hiyo.
Wakati, mnamo 2010, Kim Jong-un - mtoto wa tatu wa Kim Jong-il - alipotambulishwa kama mrithi wake dhahiri, serikali ilifanya kampeni ya kuonyesha kiongozi wa baadaye, akiwa na miaka 20 kama bingwa wa sayansi na teknolojia .
Ilikuwa ni kampeni iliyoundwa na kupata uaminifu wa kizazi chake na kuwahamasisha kuwa kiongozi huyo mdogo alikuwa ndiye shujaa wao kwa kutumia zana hizi mpya.
Kim, ambaye alichukua madaraka mwishoni mwa mwaka wa 2011 baada ya kifo cha baba yake, aliita silaha za nyuklia "upanga wa hazina", lakini pia alihitaji njia ya kuzifadhili - kazi ngumu na vikwazo vikali vilivyowekwa na Baraza la Usalama la UN baada ya majaribio ya kwanza ya nchi hiyo ya kifaa cha nyuklia na kombora la masafa marefu mnamo 2006. Udukuzi ulikuwa suluhisho moja, maafisa wa Marekani wanasema.
Kukumbatiwa kwa sayansi na teknolojia hata hivyo sio jambo lililowanufaisha Wakorea wa Kaskazini kuungana kwa njia huru kwenye mtandao wa ulimwengu, kwani hatua hiyo ingewawezesha watu wengi kuona jinsi ulimwengu unavyoonekana nje ya mipaka yao, na kufahamu tofauti kati ya mambo wanayoambiwa na kuamini na hali halisi ilivyo .
Kwa hivyo ili kuwafundisha wadukuzi wake , serikali hutuma waundaji wa programu za kompyuta wenye talanta zaidi nje ya nchi, haswa kwenda Uchina.
Huko wanajifunza jinsi ulimwengu wote hutumia kompyuta na mtandao: kununua, kucheza kamari, na kujiburudisha. Huko wao hubadilishwa kutoka kwa fikra za magwiji wa hesabu ili kuwa wadukuzi.
Wengi wa vijana hawa wanaaminika kuishi na kufanya kazi katika vituo vya nje vya Korea Kaskazini nchini China.
"Ni wazuri sana kuficha njia zao lakini wakati mwingine, kama mhalifu mwingine yeyote, wanaacha makombo, ushahidi- nyuma," anasema Kyung-jin Kim, mkuu wa zamani wa FBI Korea ambaye sasa anafanya kazi kama mpelelezi wa sekta binafsi huko Seoul. "Na tuna uwezo wa kutambua anwani zao za IP kurudi hadi waliko'
Makombo hayo yaliongoza wachunguzi kwenda kwenye hoteli moja Shenyang, kaskazini mashariki mwa China, iliyolindwa vinyago vikubwa vya simba marara wawili , mtindo wa jadi wa Kikorea. Hoteli hiyo iliitwa Chilbosan, baada ya mlima maarufu huko Korea Kaskazini.
Picha zilizochapishwa kwenye tovuti za ukaguzi wa hoteli kama Agoda zinaonyesha mandhari kama ya kikorea : vitanda vyenye rangi, vyakula vya Korea Kaskazini na wahudumu ambao huwaimbia na kuwachezea wateja wao.
"Ilikuwa inajulikana katika jamii ya majasusi", anasema Kyung-jin Kim, kwamba watuhumiwa wa udukuzi wa Korea Kaskazini walikuwa wakifanya kazi katika Chilbosan wakati walipoanza kujilikana kwa ulimwengu mnamo 2014.
Wakati huo huo, katika mji wa Kichina wa Dalian, ambapo Park Jin-hyok anaaminika kuishi kwa muongo mmoja, jamii ya waund programu za kompyuta walikuwa wakiishi na kufanya kazi katika operesheni kama hiyo inayoendeshwa na Korea Kaskazini, anasema Hyun-seung Lee aliyehama Korea Kaskazini.
Lee alizaliwa na kukulia Pyongyang lakini aliishi kwa miaka mingi huko Dalian, ambapo baba yake alikuwa mfanyabiashara mwenye uhusiano mzuri na serikali na akiifanyia kazi serikali ya Korea Kaskazini - hadi wakati familia ilipoamua kuhama nchi hiyo mnamo 2014.
Jiji hilo lilikuwa makao kwa watu wapatao 500 wa Korea Kaskazini wakati alikuwa akiishi huko, Lee anasema.
Miongoni mwao, zaidi ya 60 walikuwa waundaaji programu - vijana ambao alijua, anasema, wakati Wakorea wa Kaskazini walipokusanyika kwa likizo za kitaifa.
Mmoja wao alimkaribisha kwenye makazi yao. Hapo, Lee aliona "karibu watu 20 wanaishi pamoja na katika nafasi moja. Kwa hivyo, watu wanne hadi sita wanaoishi katika chumba kimoja, na kisha sebule waliifanya kama ofisi - kompyuta zote, zote sebuleni. "
Walimwonyesha kile walichokuwa wakiunda: michezo ya rununu ambayo walikuwa wakiuza Korea Kusini na Japani kupitia kwa madalali, wakitengeza faida ya $ 1m kwa mwaka.
Ingawa maafisa wa usalama wa Korea Kaskazini waliwaangalia sana, maisha kwa vijana hawa bado yalikuwa huru.
"Bado wamezuiliwa, lakini ikilinganishwa na Korea Kaskazini, wana uhuru mwingi ili waweze kufikia mtandao na kisha waweze kutazama sinema," Lee anasema.
Baada ya takriban miaka nane huko Dalian, Park Jin-hyok anaonekana alikuwa na wasiwasi kurudi Pyongyang.
Katika barua pepe ya 2011 iliyonaswa na FBI, anataja kutaka kuoa mchumba wake. Lakini ilichukua miaka michache zaidi kabla ya kuruhusiwa kufanya hivyo
FBI inasema wakuu wake walikuwa na misheni nyingine kwake: shambulio la mtandao kwa moja ya kampuni kubwa zaidi za burudani ulimwenguni - Sony Pictures Entertainment huko Los Angeles, California. Hollywood.
Mnamo 2013, Sony Pictures ilitangaza utengenezaji wa sinema mpya inayowahusisha Seth Rogen na James Franco ambayo ingehusisha Korea Kaskazini.
Ni juu ya mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo, aliyeigizwa na Franco, na mtayarishaji wake, aliyechezwa na Rogen. Wanaenda Korea Kaskazini kumhoji Kim Jong-un, na wanashawishiwa na CIA kumuua.
Korea Kaskazini ilitishia kulipiza kisasi dhidi ya Marekani ikiwa Sony Pictures Entertainment ingetoa filamu hiyo, na mnamo Novemba 2014 barua pepe ilitumwa kwa wakubwa wa kampuni hiyo kutoka kwa wadukuzi wanaojiita Walinzi wa Amani, wakitishia kufanya "uharibifu mkubwa".
Mnamo Mei 2017, mlipuko wa kirusi cha WannaCry ulienea kama moto wa porini, ukivuruga faili za wahasiriwa na kuwatoza fidia ya dola mia kadhaa kupata data zao, zilizolipwa kwa kutumia sarafu ya kidijital ya Bitcoin.
Huko Uingereza, Huduma ya Kitaifa ya Afya iliathiriwa vibaya sana; idara za ajali na dharura ziliathiriwa.
Wakati wachunguzi kutoka Shirika la Uhalifu wa Kitaifa la Uingereza wakichunguza udukuzi huo wakifanya kazi na FBI, waligundua kwamba virusi vilivyotumiwa kuingilia Benki ya Bangladesh na Sony Pictures vilifanana na hatimaye FBI iliongeza shambulio hili kwa mashtaka dhidi ya Park Jin- hyok.
Ikiwa madai ya FBI ni sahihi, inaonyesha jeshi la mtandao la Korea Kaskazini sasa lilikuwa limekubali sarafi za mtandani - hatua muhimu mbele kwa sababu aina hii mpya ya pesa za hali ya juu inapita mfumo wa jadi wa benki - na kwa hivyo inaweza kuzuia gharama kubwa, kama malipo kwa mawakala
WannaCry ulikuwa mwanzo tu. Katika miaka iliyofuata, kampuni za usalama za teknolojia zimeelezea mashambulizi mengi zaidi ya sarafu za kimtandao kutokea Korea Kaskazini. Wanadai wadukuzi wa nchi hiyo wamelenga malipo ambapo sarafu kama Bitcoin hubadilishwa kwa sarafu za jadi.
Kwa jumla imedaiwa wadukuzi wa Korea Kaskazini wameiba zaidi ya $ 2bn.
Na madai yanaendelea kuja. Mnamo Februari Idara ya Sheria ya Marekani iliwashtaki Wakorea wengine wawili wa kaskazini, ambao wanadaiwa kuwa wanachama wa Kikundi cha Lazaro kwa utakatishaji fedha na kuwa sehemu ya mtandao wa wizi wa pesa unaoanzia Canada hadi Nigeria.