Temitope Balogun Joshua kuzikwa leo Nigeria

0

 


Muhubiri wa Televisheni Nigeria TB Joshua anazikwa leo Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo Lagos baada ya wiki ya kutoa heshima za mwisho.

Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika katika kanisa lake la Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) lililopo kweye eneo laIkotun mjini Lagos.

Marehemu Joshua aliyekuwa na umri wa miaka 57 alifariki tarehe 5 Juni baada ya kuugua kwa muda mfupi, kulingana na kanisa.

Temitope Balogun Joshua aliheshimiwa na watu kutoka kote duniani na makumi ya maelfu ya watu walihudhuria ibada zake kila wiki.

Kupanda kwa umaarufu wake katika miaka ya 1990 kuliambatana na vipindi vya " miujiza" vilivyooneshwa kwenye televisheni za Nigeria na wachungaji.

Mafundisho yake yalitabiri uponyaji wa kila aina wa magonjwa, ikiwa ni pamoja na HIV/Ukimwi na aliwavutia watu kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.

Kilio cha TB Joshua pia kinafanyika katika kijiji cha nyumbani kwao cha  Arigidi-Akoko katika jimbo la Ondo
Image caption: Kilio cha TB Joshua pia kinafanyika katika kijiji cha nyumbani kwao cha Arigidi-Akoko katika jimbo la Ondo

Akifahamika kama "Nabii" miongoni mwa wafuasi wake, alimiliki televisheni ya Kikristo - Emmanuel TV na mara kwa mara alitembelea Africa, Marekani, Uingereza and na Amerika Kusini.

Bw Joshua alitoka katika familia masikini na alilelewa na mjomba wake kufuatia kifo cha baba yake Mkristo.

Wachungaji wengine maarufu ambao hawakuhudhuria ibada za wiki hii za kumuombea Bw Joshua, walielezea kutokuwa na mahusiano mazuri nae.

Wafuasi wa Bw Joshua walimtambua kama mtu aliyekuwa na haiba na mnyenyekevu,
Image caption: Wafuasi wa Bw Joshua walimtambua kama mtu aliyekuwa na haiba na mnyenyekevu,

Jumuiya ya Wakristo wa Nigeria (Can) na ule wa makanisa ya Kipentekoste nchini Nigeria (PFN) awali walimuelezea Bw Joshua kama"mpotofu"ambaye anatoka katika kikundi cha "wachawi" ambaye ameiuingilia Ukristo.

Can hatahivyo imetoa taarifa siku chache kabla ya kifo chake, ikisema " kifo chake ni hasara sit u kwa familia na kanisa, bali kwa Nigeria na dunia nzima kwa ujumla ".

TB Joshua

Wafuasi wa Bw Joshua walimtambua kama mtu aliyekuwa na haiba na mnyenyekevu, na maelfu wanatarajiwa kujitokeza katika mazishi yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable