Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameshindwa katika azma ya kuzuia kukamatwa kwake - ikimaanisha kuwa ataendelea kubakia gerezani.
Mawakili wa Bw Zuma wanamatumaini ya kubadilisha hukumu ya miezi 15 kwa kutoheshimu agizo la mahakama, ambayo alianza kuitumikia wiki hii baada ya kujipeleka katika kituo cha polisi Jumatano jioni.
Lakini akizungumza Ijumaa, jaji aliyeongoza kesi alisema ombi lake "limepuuziliwa mbali kwa gharama".
Hatahivyo, hili sio jaribio pekee alilolifanya Zuma la kutaka kubadilishwa kwa hukumu dhidi yake iliyotolewa na mahakama ya katiba ya Afrika Kusini baada ya kushindwa kuhudhuria kikao cha uchunguzi wa madai ya ufisadiuliofanyika wakati wa uongozi wake.
Anakana kuhusika na ufisadi wowote, na hajaonesha ushirikiano na mahakama..
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Nomsa Maseko, kesi hiyo inatarajiwa kurejeshwa tena katika mahakama ya katiba Jumatatu, wakati ambapo majaji wataangalia iwapo wataendeleza hukumu au kuipunguza.
Kwa sasa Zuma, ambaye bado ana ufuasi mkubwa nchini Afrika Kusini, atakuwa na haki ya kupata msamaha katika kipindi cha chini ya miezi, kulingana na maafisa.
