Tetesi za soka Ulaya Jumapili 04.07.2021: Messi, Van de Beek, Saul, Johnstone, Pogba, Ziyech, Coutinho

 

Lionel Messi yuko huru baada ya mkataba wake na Barcelona kufikia kikomo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Paris St-Germain wametoa ofa ya mkataba kwa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, ambaye sasa yuko huru baada ya mkataba wake na Barcelona kufikia kikomo. Hatahivyo, Barcelona ina matumaini ya kuendelea kusalia naye mchezaji huyo. (AS-in Spanish)

Manchester United wako tayari kumuachia Donny van de Beek aondoke klabuni hapo wakati Real Madrid ikimtaka kwa mkopo kiungo huyo wa kati wa Kiholanzi mwenye miaka 24.(Star)

Kuondoka kwa Van de Beek kunaweza kufungua njia kwa United kumsajili mlinzi wa kati Raphael Varane,28 anayekipiga klabu ya Real Madrid. (Sun)

Manchester United wako tayari kumuachia Donny van de Beek

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Liverpool inatazama mpango wa uhamisho wa kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez,26, huku Mhispania huyo akiwa na mpango wa kucheza ligi ya Primia.

Arsenal wako tayari kufikiria uhamisho wa mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone,28, ikiwa dili lake kwa Aaron Ramsdale,23, wa Sheffield United, halitafanikiwa. (Star)

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Liverpool pia inamtaka kiungo wa kati wa Lille Renato Sanches,23, lakini watakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal. (Onze Mondial-in French)

Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ameitaarifu klabu kuhusu shauku yake ya kumsaini tena Paul Pogba kutoka Manchester United . Mchezaji huyo , ambaye mkataba wake Old Trafford utakwisha mwaka 2022, alishinda mataji mawili ya Serie A akiwa na Juve wakati Allegri akikiongoza kikosi hicho. (90 Min)

Hakim Ziyech anatakiwa na AC Milan, wanaomwona kiungo mchezeshaji wa Chelsea raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 28 kama mle anayeweza kufikiwa zaidi kuliko James Rodriguez wa Everton kutokana na madai ya mshahara wa mchezaji huyo mwenye asili ya Colombia.(Corrier dello Sport via Sport Witness)

Paul Pogba

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hatahivyo, Milan pia wamepewa ofa ya mshambuliaji Philippe Coutinho na Barcelona, ambao wana mpango wa kumuondoa nyota wa zamani wa Liverpool. (Mundo Deportivo-in Spanish)

Kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard,22, amethibitisha kuwa hatarejea Arsenal msimu ujao baada ya kucheza kwa mkopo jijini London akitokea Real Madrid. (Football London)

Kocha wa Burnley Sean Dyche anaandaa zabuni kumsajili winga Marc Albrighton kutoka Leicester. (Sun)

Kiungo wa kati wa Norway anayekipiga Real Madrid Martin Odegaard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

AC Milan inamnyemelea mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Jamhuri ya Czech Patrik Schick.(Tuttomercatoweb - in Italian)

Inter Milan wameanza mazungumzo na wakala wa Denzel Dumfries kwa matumaini ya kumnasa mchezaji huyo wa PSV Einndhoven. (Calciomercato via Football Italia)

Denzel Dumfries

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tottenham wana nia ya kumnasa mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic,21, lakini mchezaji huyo raia wa Serbia anatazamia kupata mkataba mpya na klabu hiyo ya Serie A baada ya kufunga magoli 21 katika michezo 37 aliyocheza mwaka 2020-2021. (Corriere dello Sport via Sport Witness)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mfaransa Matteo Guendouzi, 22, anakaribia kuhamia Marseille na kilabu cha Ligue 1 pia kinatarajiwa kukamilisha mpango wa mlinzi wa Gunners William Saliba, 20. (Goal)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post