Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 05.07.2021: Pjanic, Umtiti, Ronaldo, Mendy, Ryan, Willock

 

Cristiano Ronaldo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo

Wakala wa Cristiano Ronaldo Jorge Mendes anafanyia kazi mpango wa kuongezwa kwa mkataba nyota huyo wa kusalia Juventus kwa mwaka mmoja zaidi utakaomfunga mshambuliaji huyo wa Ureno kuendelea kukipigia klabu hiyo ya Serie A mpaka mwaka 2023. Hivyo klabu ambazo zilikuwa zinamyatia mshambuliaji huyo kama Man United itabidi zisubiri mpaka 2023. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Barcelona wako tayari kukatisha mikataba ya wachezaji wake Mbosnia Miralem Pjanic, 31 na mlinzi Mfaransa Samuel Umtiti, 27 ambao wanaonekana hawako kwenye mipango ya Meneja Ronald Koeman. (Goal)

Pjanic anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Tottenham, ambao wanaotaka kumsaini kuwapiku Manchester United wanaomuhusudu kwa muda mrefu kiungo huyo. (Express)

Barca
Maelezo ya picha,

Umtiti anadaiwa kuwa hayupo kwenye mipango ya baadae ya kocha wa Barcelona

Tottenham na Barcelona wanamuwania nahodha wa Napoli Lorenzo Insigne, ambaye ameng'ara katika michuano ya Euro 2020, mkataba wake unaisha mwaka 2020 na mpaka sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 hajasaini mkataba mpya (Corriere dello Sport - in Italian)

Barcelona wako tayari kupokea ada kiduchu kwa ajili ya kiungo wake Mbrazil Philippe Coutinho kuliko ile waliyoilipa Liverpool wakati nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alipojiunga na wakali hao wa La Liga, thamani yake inaendelea kushuka.

Barca
Maelezo ya picha,

Kiwango cha Coutinho kimeendelea kuporomoka na kushusha thamani yake

Mlinda mlango wa Brighton Mat Ryan, 29, ambaye aliichezea Arsenal kwa mkopo msimu uliopita anakaribia kutua Real Sociedad baada ya ada ya uhamisho wa Muastralia huyo ambayo haijafahamika kukubalika. (Sky Sports)

Mlinzi wa zamani wa Newcastle Steve Howey anasema klabu hiyo lazima imsajili kiungo wa kiingereza Joe Willock, 21, msimu huu au wawe katika hatari ya kumkosa kabisa huko mbeleni kwa sababu ya vita bei ya nyota huyo wa Arsenal. (Chronicle)

Mlinzi wa kushoto wa Manchester City, mfaransa Benjamin Mendy, 26, anatajwa kuwa kwenye orodha ya nyota wanaotakiwa na Inter Milan msimu huu. (Manchester Evening News)

Mendy

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mendy

Manchester United itamgeukia mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde,22, kama mbadala wa Raphael Varane, 28, iwapo klabu hiyo ya Ligi kuu ya England itashindwa kumsajili mlinzi huyo kutoka Real Madrid. (AS - in Spanish)

Mlinzi wa kushoto wa Barcelona Mhispania Junior Firpo, 24, anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa kudumu kujiunga na Leeds United. (The Athletic - subscription required)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post