Kile ambacho familia imekipitia mwishoni mwa mwezi Juni, kilikuwa cha kutisha na kigumu sana.
Watu wanne waligongwa na gari ambalo walikuwa wanasafiri nalo kutoka mji wa Monterrey kuelekea Nuevo Laredo , kaskazini-mashariki mwa Mexico, na kutelekezwa katikati ya barabara.
"Wana hali gani? Wazima?" Aliuliza dereva, wakati shambulio hilo liliporekodiwa kwa mbali.
"Ilikuwa inaogopesha , baba alijibu , ambaye baadae aliviambia vyombo vya habari kuwa watu wawili wenye silaha walitoka nje ya gari wakiwa na bunduki."
Mbele yao waliwatoa wapenzi nje ya gari nyeupe ya 'pick up' na baada ya hapo , mtu mmoja mwenye silaha alikuja mbele yangu, alikuwa kama ana miaka 30, alisema mtu ambaye hakutaja jina lake kwasababu za kiusalama.
"Kaa chini! na weka simu yako chini!"Alitoa agizo.
"Familia yangu yote ilikuwa inatembea kwa kurudi nyuma."
Lakini kwanini familia hiyo ilikuwa na hofu. Familia nyingi zimepoteza wapendwa wao kutokana na hali ya kiusalama kutokuwa nzuri.
Na ilikuwa suala la kusafiri ukitoka Monterrey - mji ambao ni muhimu wa viwanda nchini Mexico - kuelekea mpaka wa mji wa Nuevo Laredo limekuwa eneo hatari.
Barabara yenye urefu wa kilomita 200, miezi ya hivi karibuni imekuwa ikiitwa barabara kuu ya ugaidi kutokana na ongezeko la matukio ya utekaji na watu kupotea.
Kwa mujibu wa kikosi cha pamoja cha kusaka waliopotea huko Nuevo León (FUNDENL) taasisi kubwa inayosaidia wakazi
Watu wapatao 49 wamepotea mwaka huu katika jimbo hilo pekee.
Ni idadi kubwa ya watu ukilinganisha na miaka 10 iliyopita, Angélica Orozco,msemaji wa taasisi hiyo, aliiambia BBC.
"Wanawavamia wananchi moja kwa moja, ambao hawana hatia na hawana taarifa ya chochote kwasababu hawatutaarifu kile kinachotokea, "alisema.
Mamlaka ya Nuevo León, kwa sehemu yao, wametoa taarifa ya kiuchunguzi kwa watu 41 ambao wamepotea ndani ya miezi 20, kwa wastani wa 1.4 kwa kila tukio.Na wametangaza hatua mpya ambazo
watachukua katika msako wao.
Lakini taasisi ya FUNDENL na taasisi nyingine zimetoa angalizo kuwa inawezekana kuna matukio mengine ambayo taarifa hazijawafikia.
Barabara ya kisasa na hatari
Barabara inayohusisha Monterrey na Nuevo Laredo si barabara kuu lakini imedhibitiwa na makundi ya kihalifu katika maeneo yenye mzozo nchini Mexico.
Mambo ni tofauti kabisa , ni barabara kuu ya njia nne, vibanda vya kielektroniki na vilevile miundo mbinu ni mizuri katika safari moja tu.
Ni sehemu ya barabara ya Pan-American, ambayo inakutanisha bara la Amerika kutoka upande wa kaskazini mpaka kusini.
Katika njia ndefu kutoka Mexico ya kati kuelekea mpakani mwa Marekani, ni njia muhimu, katika usafirishaji na utumaji mizigo nje ya nchi pamoja na watalii wa Monterrey ambao huwa wanaenda katika miji ya kusini kwa ajili ya utalii na biashara kutoka Texas.
"Hiyo ni njia ya mpaka wa watu wanaoenda Marekani kwa ajili ya manunuzi au sababu zao binafsi.
Na ndio maana tunaamini kuwa mamlaka ina taarifa kwa miaka kadhaa kuhusu kupotea kwa watu.
Na hakuna picha ya video au operesheni inayoendelea,"Orozco aliainisha.
Licha ya kwamba miundombinu kuwa mizuri lakini hakuna usalama kwa madereva na wenyeji.
Hakuna uhakika wa operesheni yeyote."
Ongezeko kubwa la hatari
Haswa , katika hali ambayo ilikuwa hatari sana katika miezi ya hivi karibuni.
Huu ni mpaka kati ya Nuevo León na Tamaulipas.
Juni 19, mhandisi mwenye miaka 35 - ambaye hataki jina lake litajwe alikuwa ametekwa kwa saa kadhaa na watu waliovaa sare za jeshi wakiwa na silaha.
Katika malalamiko kwa wizara ya Umma ya Nuevo León alisema kulikuwa na kizuizi cha watu wenye silaha.
Walimuweka ndani ya gari , huku akiwa amefunika kichwa siku nzima na kumsukuma barabarani.
Walimuuliza, je dawa za kulevya zimeleta athari gani na anafanyia kazi nyumbani na haifahamiki anamfanyia nani kazi .
Licha ya kuwa , licha ya ukweli kuwa wanafanya kazi kwa mujibu wa mfumo wa kampuni na alikuwa na kazi ya data katika simu.
Katika usafirishaji wa dawa na bidhaa haramu, pamoja na rasilimali za kiuchumi , alieleza VÃctor Sánchez .
Alieleza kuwa mwisho wa siku wanaachiwa huku macho yakiwa yamefunikwa.
FUNDENL imebaini kwamba madereva ambao wako kwenye hatari zaidi ni waendesha Uber au Didi, ambapo aliomba kufanya safari katika mpaka, vilevile wamekuwa wana mashambulizi mpakani au magenge ya wahalifu pia yaliwashambulia.
"Kwa ujumla , kuna makala yake tangu mwaka 2011. Na kukiwa na majanga tangu mwaka uanze," alifafanua Orozco.
Siku za hivi karibuni makundi mengi ya kihalifu yameibuka katika maeneo ya mipaka ya Marekani katika jimbo la Tamaulipas, Nuevo León na Coahuila.
Ni maeneo muhimu katika usafirishaji wa dawa za kulevya, bidhaa za kimagendo na rasilimali za kiuchumi, alieleza mtafiti VÃctor Sánchez.
Sehemu ya eneo hilo la barabara karibu na Sabinas Hidalgo , ni la hatari sana.
Ingawa kumekuwa na watu wanafanya biashara hizo haramu kwa miongo kadhaa lakini hali imekuwa mbaya kwa siku za hivi karibuni.
Hali hiyo imefanya eneo hilo kuwa na hali ya mizozo na ghasia.
Serikali imejibu nini
Kutokana na upoteaji wa watu, serikali imeanza kuchukua hatua hivi karibuni.
Kuna askari kadhaa wanalinda kwa sasa.
Na wiki iliyopita , gavana wa Nuevo León na Tamaulipas walikutana na kukubaliana katika kuratibu uchunguzi wa kesi za watu kupotea.Hilo ndilo jambo ambalo wahanga wanataka.
Serikali ya Nuevo León imesema itachukua hatua mpya kukabiliana na matukio ya watu kupotea.
Orozco, alitoa angalizo kuwa hizi hatua huwa za muda mfupi mara nyingi . Wakiondoka na tatizo linarudi kuwa lilelile.
"Na mbinu wanayoitumia serikali ni sawa tu na mashambulizi ya makundi ya wahalifu ambao wanawavamia wafanyakazi na familia zao, inasikitisha."