Usalama wa rais:Wafahamu marais ambao wameponea kuuawa katika siku za hivi karibuni

 

haiti

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Usalama wa rais wa nchi yoyote huwa suala muhimu ambalo huchukua raslimali nyingi na mipango ya muda mrefu ili kuto hakikisho kwa umma kwamba kiongozi wan chi yuko salama .

Hata hivyo pametokea visa vya marais kuuawa wakiwa madarakani na hata wengine kuponea kupitia majaribio ya kuwaua wakiwa wangali madarakani

Hivi Karibuni-tarehe 20 mwezi Aprili mwaka huu , Afrika na ulimwengui ilipokea Habari za kutisha na za ghafla kwamba rais wa Chad Idriss Deby aliuawa .

Wengi walitaka kujua hali iliyopelekea mauaji ya rais huyo na serikali ya Chad ilitoa taarifa kueleza kwamba Deby alikuwa katika mstari wa mbele kupambana na waasi wakati alipokumbana na mauti yake kwa kupigwa risasi

Kisha Katika tukio jingine la mauaji ya rais, Kiongozi wa Haiti Jovenel Moise aliuawa mnamo Julai tarehe 7 mwaka huu katika shambulio dhidi ya makazi yake mjini Port-au-Prince .

Jovenel Moïse, 53, alikuwa madarakani tangu Februari 2017, baada ya mtangulizi wake, Michel Martelly kung'atuka mamlakani.Tayari mamlaka nchini humo zimewakamata watu kadhaa wakiwemo wanajeshi wastaafu kutoka Colombia na watu wawili wanaodaiwa kuwa rais wa Marekani .

Mauaji hayo yanatoa taswira jinsi kazi ya urais inavyoweza kuwa hatari wa maisha ya mtu na hata familia yake na kando na viongozi hao ambao wameuawa siku za hivi karibuni ,kunao ambao wamenusurika majaribio ya kuwaua.Hii hapa orodha na maelezo ya viongozi wa nchi waliozuia mjaribio ya kuwauwa wakiwa madarakani

Andry Rajoelina-Madagascar

Madagascar wiki jana ilitangaza kwamba ilizuia njama ya kumuua rais Andry Rajoelina na kuwakamata watu sita wawili kati yao wakiwa raia wa Ufaransa .

"Wageni kadhaa na raia walikamatwa Jumanne, Julai 20, kama sehemu ya uchunguzi wa shambulio la usalama wa serikali," mwendesha mashtaka Berthine Razafiarivony alisema katika taarifa.

rajo

CHANZO CHA PICHA,AFP

"Kulingana na ushahidi tulio nao, watu hawa walipanga mpango wa kuwauwa viongozi kadhaa nchini pamoja na mkuu wa nchi," alisema, bila kutoa maelezo juu ya operesheni hiyo.

Waziri wa Usalama wa Umma Fanomezantsoa Rodellys Randrianarison alisema watu sita wamekamatwa, wakiwemo "mgeni, raia 2 wenye uraia wa nchi mbili na wamadagaska watatu."

"Polisi walikuwa na habari juu ya jambo hili kwa miezi," aliambia mkutano wa waandishi wa habari.

Walianza kukamatwa kwa wakati mmoja katika maeneo tofauti na tukanasa pesa na silaha' alisema.

Tangazo la njama ya mauaji linakuja baada ya miezi kadhaa ya ghasia na vitisho kwa waandishi wa habari wanaoripoti juu ya janga la corona nchini humo na baa la njaa kusini mwa nchi.

Katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Madagaska mnamo Juni 26, askari walitangaza kuwa wametibua jaribio la kumuua bosi wao, Jenerali Richard Ravalomanana, ambaye ni mshirika wa karibu Rajoelina.

Mnamo Aprili, vipindi tisa vya Televisheni na redio vilizuiwa kwa sababu "vililenga kusumbua utulivu wa umma na usalama na kudhuru umoja wa kitaifa."

Rivo Rakotovao, rais wa zamani wa muda, alisema alilaani aina yoyote ya jaribio la mauaji lakini aliogopa kuwa tangazo hilo linaweza kuwa chanzo rais Rajoelina kuzidisha ukandamizaji

Assimi Goita-Mali

Rais wa mpito wa Mali Kanali Assimi Goita, ambaye alichukua madaraka mnamo Juni baada ya kuongoza mapinduzi - ya pili chini ya mwaka mmoja - yuko salama baada ya kile ofisi yake ilitaja kama jaribio la mauaji. Wanaume wawili, mmoja na kisu, walimshambulia Goita Jumanne wiki jana baada ya sala kwenye Msikiti Mkuu wa Bamako kwa sherehe ya Eid al-Adha, inayojulikana kama Tabaski, Afrika Magharibi.

goita

CHANZO CHA PICHA,AFP

Ofisi ya rais ilisema shambulio hilo lilikuwa jaribio la mauaji, na kwamba Goita alikuwa "salama " katika kambi ya kijeshi ya Kati nje ya mji mkuu, "ambapo usalama umeimarishwa."

Wanaume hao walimshambulia Goita wakati imamu alipokuwa akiwaelekeza waumini nje ya msikiti kwa kafara ya wanyama, kama sehemu ya sherehe.

"Mara moja mshambuliaji alizidiwa nguvu na maafisa wa usalama. Uchunguzi unaendelea," ikasema ofisi ya rais .

Goita aliwaongoza maafisa wengine wa jeshi katika mapinduzi ya Agosti kushinikiza rais Ibrahim Boubacar Keita kuondoka madarakai , kufuatia wiki kadhaa za maandamano makubwa juu ya ufisadi.

yalikuwa ni mapinduzi ya pili katika miezi tisa, na yalisababisha Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi kuifurusha Mali , wakitaka uteuzi wa waziri mkuu ambaye ni raia.

Jeshi lilikabidhi nguvu kwa serikali ya mpito inayoongozwa na raia, ambayo iliteua maafisa wa jeshi katika majukumu muhimu.

Goita, kama rais wa mpito, aliahidi "uchaguzi wa kuaminika, wa haki na wa uwazi" na makabidhiano ya utawala kwa raia ifikapo Juni 2022.

Ufaransa, ambayo ina maelfu ya wanajeshi waliopo nchini kusaidia mapigano dhidi ya makundi ya kijihadi, ilisitisha ushirikiano wa kijeshi baada ya mapinduzi, na baadaye ikatangaza kuwa italiondoa jeshi la Barkhane ambalo limekuwa likipambana na wanajihadi huko Sahel tangu 2013.

Abiy Ahmed-Ethiopia

Mnamo Juni mwaka wa 2018 miezi mitatu tu baada ya kuchukua madaraka waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alinusurika katika shambulio la gruneti katika mkutano wa kisiasa wa wafuasi wake kumuunga mkono kuhusu mageuzi aliyokuwa ameanzanisha nchini humo .

Abiy

CHANZO CHA PICHA,AFP

Abiy, ambaye miezi yake mitatu ya kwanza afisini ilitoa ishara za mageuzi makubwa ikiwemo kuifungua nchi kwa ulimwengu na kuafikia mapatano na nchi jirani ya Eritrea alikimbizw ahadi eneo salama na walinzi wake muda mfupi baada ya shambulio hilo.

Mwanajeshi huyo wa zamani alisema shamulio hilo lililosababisha kifo cha mtu mmoja lililenga kuligawanya taifa .Polisi baadaye walisema watu sita walikamatwa lakini maelezo kamili hayakutolewa .

Abiy alikuwa amechukua hatamu mwezi Aprili mwaka huo akiahidi kuleta uwazi ndani ya serikali ya kufanikisha taratibu zote za kuwapatanisha waethiopia.Hata hivyo tangia wakati huo mengi yamebadilika kwani licha ya kushinda tuzo ya Amani ya Nobel Abiy alitangaza vita baadaye dhidi ya chma cha TPLF na mzozo huo unaendelea kuenea nchini mwake .Alitofautiana kisiasa na waliokuwa wakuu wa TPLF ambao walihamakishwa na baadhi ya mageuzi aliyoleta ambayo yaliwaondoa kutoka nafasi za ushawishi serikalini .

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post