Virusi vya corona: Jinsi 'janga la watu wasiochanjwa' linavyoikabili Marekani

 

Una mujer recibe una vacuna en EE.UU.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ugonjwa virusi vya corona unachukua sura mpya na janga hilo sasa linaelekea "katika njia isiyo sahihi" nchini Marekani.

Tahadhari hiyo imetolewa na mshauri mkuu wa magonjwa ya kuambukiza wa rais wa Marekani, Dkt Anthony Fauci ambaye awali alionya kuwa janga la corona lingerejea upya Marekani kama hatua stahiki zisingechukuliwa mapema.

Kufikia sasa watu waliochanjwa nchini Marekani ni chini ya nusu ya raia wote wa nchi hiyo. Taifa hilo ndilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu waliofariki kutokana na janga la corona na mustakabali wake wa hali ya mambo unatia mashaka.

Katika wiki ya mwisho ya Juni, nchi hiyo iliandikisha wagonjwa 92,000, lakini idadi hiyo imepaa mpaka zaidi ya 500,000 katika siku saba zilizopita.

Kusambaa kwa kirusi kipya cha corona aina ya delta ni moja ya sababu ya ongezeko hilo kubwa la maambukizi, zaidi ya hilo kuna suala la kusuasua kwa utolewaji wa chanjo, hususani kwenye majimbo ya wahafidhina ya kusini mashariki mwa nchi hiyo.

"Kwa kweli ni janga la watu wasiochanjwa," Fauci ameambia CNN.

Kiini cha tatizoWatu wasiochanjwa

Hivi karibuni mganga mkuu wa Marekani, Vivek Murthy, alibainisha kwamba asilimia 99.5 ya vifo vitokanavyo na corona nchini humo ni vya watu ambao hawajachanjwa.

Anthony Fauci

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

"Kwa kweli ni janga la watu wasiochanjwa," amesema Anthony Fauci.

Dkt Marcus Plescia, ambaye ni mkurugenzi wa umoja wa watoa huduma za afya wa majimbo ameieleza BBC kuwa ongezeko hilo la maambukizi limeshamiri katika eneo moja la nchi hiyo.

"Ni tatizo kubwa katika majimbo sita ama saba hivi. Majimbo ya kusini mashariki na baadhi ya majimbo ya kati magharibi," amesema Plescia.

Alabama, Mississippi, Arkansas, Georgia, Tennessee, Oklahoma ni majimbo ambayo waliochanjwa ni chini ya asilimia 40, ukilinganisha na majimbo ya kaskazini mashariki kama Vermont na Massachusetts ambapo waliochanjwa ni zaidi ya asilimia 65.

Jambo la muhimu kuzingatia ni kuwa, magavana wa majimbo yenye wastani mdogo wa watu waliochanjwa - wengi wao ni kutoka chama cha Republicans - tayari walishaonesha wasiasi na kebehi juu ya hatua za serikali kuu toka mwaka jana.

"Ni tatizo hususani la watu ambao hawajachanjwa, na hiyo ndiyo sababu tunawaomba watu wasiochanjwa wajitokeze na kuchanja," ameeleza.

Kukwama kwa chanjo

Promotores de la vacunación en Alabama

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jimboni Alabama, mamlaka zinapigia chapuo chanjo ya mlango kwa mlango.

Viwango vya uchanjaji nchini Marekani vimekwama katika miezi ya hivi karibuni.

Marekani imekuwa na viwango vya juu zaidi vya utoaji wa dozi za chanjo duniani katika mwezi wote wa Aprili, lakini tangu wakati huovimepungua kwa kuwango kikubwa.

Idadi ya watu ya watu waliochanjwa hadi sasa nchini Marekani ni takriban milioni 163, sawa na asilimia 49 ya idadi ya watu wa nchi hiyo( takriban asilimia 18 ya watu wa nchi hiyo wana chini ya umri wa miaka 12, ambao hawajaidhinishwa kupewa chanjo).

Plescia anasema kwamba nchi hiyo imeanza kusajiri "ongezeko kidogo la juu" katika kiwango cha uchangjaji baada ya taaarifa za hivi karibuni zinazoonesha ongezeko la maambukizi ya corona miongoni mwa watu ambao hawakuchanjwa.

"Tungependa kuona zaidi ongezeko hilo, lakini tunaona dalili za kuongezeka kidogo na tunasikia kutoka kwa watu kwamba maambukizi ya hili wimbi jipya yamevuta hisia zao," hasa miongoni mwa wale ambao walikuwa tayari kuangalia uwezekano wa kuchanjwa, sio sana miongoni mwa wale walioikataa, anaeleza.

Katika mahojiano na CCN , Faucci alisema kuwa viongozi wa kieleo katika maeneo yenye viango vya chini vya uchanjaji wanapaswa kuwatia moyo zaidi watu wapate dozi za chanjo.

Sasa Mavana wa Republican wa Arkansas na Florida - ambao waliukosoa ushauri wa Fauci siku zilizopita- wamekuwa wakihamasisha watu wapate chanjo katika majimbo yao.

Kusambaa kwa aina ya virusi ya Delta

Tatizo linaloambatana na viwango vya chini vya uchanjaji katika baadhi ya majimbo ya Marekani limekuwa ni kusambaa kwa aina mpya virusi vya corona ya delta SARS-CoV-2.

Kwa kuwa inaambukiza zaidi kuliko aina nyingine, kirusi hiki kimesambaa kwa kasi zaidi miongoni mwa watu ambao hawajapata dozi yoyote ya chanjo, kama ilivyoelezwa na maafisa wote na wataalamu wa afya kwa pamoja.

coronavirus

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

"Hapo ndio tunaona uhalisia wa ongezeko hilo. Katika maeneo mengine ambako viwango vya chanjo ni vya juu, hatuoni tatizo kubwa, ingawa hata majimbo hayo tunaanza kuona ongezeko. Mambo yanaibuka," anasema Dkt Plescia.

Majimbo ambayo hayakubaki nyuma katika uchanjaji, kama vile Florida (48.7), ni miongoni mwa yale ambayo yalioyanza kushuhudia idadi ya wanaopatwa na maambukizi au hata kulazwa ikipanda mara mbili au hata mara tatu.

Wakati mwanzoni mwa janga ilikuwa haijulikani kwamba mtu anaweza kuwa ameambukizwa kwa kuwa dakika 15 mbele ya mtu mwenye maambukizi asiye na barakoa, kulingana na mtaalamu wa magonjwa yanayoambukizwa Celine Gounder, aina ya delta husambaa kwa kasi kubwa zaidi.

Kutovaa barakoa

Tofauti na mwaka jana, msimu huu wa kiangazi, Wamarekani wamerejea likizoni, wakihudhuria matamasha na matukio ya michezo, au wakila chakula katika migahawa yenye umati wa watu bila kuvaa barakoa au kuzingatia mwongozo wa kukaa mbali baina yao.

Kuondolewa kwa miongozo hiyo kuliongezeka haraka kuanzia tarehe 13 Mei, wakati rais wa Marekani, Joe Biden, aliposema kwamba wale ambao wamepata chanjo kamili wanaweza kurejea katika maisha yao ya kawaida bila kutumia barakoa.

Joe Biden quitándose la mascarilla

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Joe Biden alisema, "Ni siku nzuri kwa Marekani" katika kutangaza mwisho wa sera ya barakoa kwa waliochanjwa mwezi Mei.

Lakini sasa wakati janga limeibuka upya, maafisa wameanza kujiuliza iwapo ni muhimu kurejea kwenye sera ya zamani.

"Tunaona hilo linatokea Los Angeles. Tunaona hilo Chicago. Tunashuhudia hilo pia New Orleans," Fauci aliiambia CNN. "Maafisa pale, wengi wao, wanasema hata kama umechanjwa ni busara kuvaa barakoa ndani ya maeneo yaliyofungwa na ya mkusanyiko."

Plescia, kwa upande wake anaamini kuwa chanjo ni suluhu bora zaidi ya barakoa.

Bañistas en Miami Beach

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Fukwe za Miami zimekuwa zikifurika watu hawafuati tena maagizo ya kupambana na covid-19.

"Kulingana na tunavyojua kutokana na sayansi, hiyo ndio sera thabiti. Ninamaanisha watu ambao wamepata chanjo kamili, kwasabbu tuna chanjo nzuri sana. Zina ufanisi sana, sana, kwa bahati nzuri," aliiambia BBC.

"Hata katika maambukizi [ya virusi aina ya delta], watu hawa hawawezi kuugua sana au kulazwa hospitalini au kufariki ," aliongeza.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post