Jeshi la polisi nchini Tanzania limetangaza Oparesheni ya usalama inaendelea katika Mji wa Kibiti umbali wa kilomita 150 na jiji la kibiashara Dar es salaam.
Jeshi hilo limesema limekusudia kuwafukuza wahalifu, pamoja na watu kutoka vikundi vya ugaidi wanaokimbia operesheni za usalama nchini Msumbiji.
Hatua hii inakuja wakati huu ambapo mapambano dhidi ya magaidi katika jimbo la kaskazini la Msumbiji Cabo Delgado yakipamba moto na majeshi kutoka nchi nyengine za kiafrika kama Rwanda yakisaidiana na vikosi vya Msumbiji kwenye mapambano hayo.
Kampuni ya mafuta ya Ufaransa ilisitisha shughuli zake katika eneo hilo kufuatia kukithiri kwa vurugu na mashambulizi ya wanamgambo mnamo Machi 2021.
Mwandishi wa BBC Martha Saranga amezungumza na Simon Siro inspekta jenerali wa polisi nchini Tanzania.