Polisi yaua wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi Lindi

0

 

wauwapic

Kamanda wa polisi kamishina msaidizi wa jeshi la polis Mtatiro Kitinkwi

Lindi. Watu wane kati ya sita wanaosadikiwa kuwa jambazi wameuwawa baada ya kutokea kwa mapigano ya kurushiana risasi na jeshi la polisi mkoani hapa.

Tukio Hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia jana Agosti 6, 2021 katika Kijiji cha Nanganga wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Kamishina Msaidizi Mtatiro Kitinkwi amesema jana kuwa walipata taarifa za kintelijensia za kuwepo kwa kundi la majambazi linaloelekea kufanya tukio katikati ya Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea barabara ya Nanganga.

Amesema, kwa kutumia doria ya pikipiki, waliweka mtego katika maeneo hayo.

Kamanda Mtatiro amesma baada ya muda  zilitokea pikipiki mbili zilizokuwa zimepakia mishikaki kila moja ilikuwa  na abiria wawili , wawili, waliposimamishwa Kwa lengo la kuhojiwa walikaidi na ndipo walianza kurushiana risasi na Polisi.

Katika majibizano hayo ya risasi, anasema watu wanne walijeruiwa na kukimbizwa hospital ya mkoa ya Sokoine wakiwa njiani walipoteza maisha.

Kamanda Mtatiro ametoa onyo kali kwa wahalifu wanaojaribu kuja kufanya uharifu katika mkoa Lindi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable