Kufuatia hatua ya leo ya Korea Kaskazini kufyatua kombora la masafa marefu Marekani imelaani kitendo hicho na kuitaka Serikali ya Taifa hilo kujiepusha na vitendo vya kudhoofisha zaidi hali ya utulivu
Taarifa za ndani za Korea Kaskazini zinaonesha kuwa Taifa hilo linajiandaa na maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 110 ya kuzaliwa kwa Mwasisi wake Kim Sung II yanayaotarajiwa kufanyika April 2022 ambapo inasemekana Serikali ya Pyonyang inaweza kuitumia kufanya majaribio ya silaha nzito zaidi.
