Kutoka Urusi Rais Vladimir Putin ametoa amri kwa Jeshi la Nchi hiyo kuweka vikosi vya kuzuia nyuklia vya Urusi katika hali ya tahadhari baada ya kauli zilizotolewa na Viongozi wa Nchi za NATO.
Akizungumza kwenye Televisheni ya Taifa Rais Putin amesema "Kama unavyoona, sio tu kwamba Nchi za Magharibi huchukua hatua zisizo za kirafiki dhidi ya Nchi yetu katika nyanja ya kiuchumi, namaanisha vikwazo haramu ambavyo kila mtu anavijua vyema lakini pia Maafisa Wakuu wa Nchi zinazoongoza NATO wanajiruhusu kutoa matamshi ya kichokozi kuhusiana na Nchi yetu"
