BAADHI YA WATANZANIA WAANZA KUONDOKA UKRAINE, TRENI ZIMEJAA WENGINE WAMEKAA CHINI.......

0

 

 


 

 

Kwa mujibu wa Mtanzania aliefanya mahojiano na kituo cha Millard Ayo ameeleza kuwa Baadhi ya Watanzania waliopo Nchini Ukraine wameanza kuondoka kwenye Nchi hiyo kukimbilia Nchi jirani ya Poland ambapo mmoja wao aitwae Nenyo ambaye ni Mwanafunzi amesema kwamba wamebahatika kupanda Treni ya Serikali ambayo imetumwa kuokoa Watu na kuwapeleka Nchi jirani.
 
"Tupo kwenye Treni sasa hivi, imejaa kwa kubanana na Watu wengine wamekaa chini wengine wamesimama, ni Treni ya bure iliyotolewa na Serikali kuokoa Watu na Watu ni wengi hivyo Treni ni ya kugombania"
 
"Sio Watanzania wote tumefanikiwa kuingia kwani wengine walishindwa kupenya na sisi tulioingia imejaa mpaka tumekaa chini, tunaelekea Mji wa Iviv kisha kwenda Nchini Poland baada ya hapo, safari tu ya kwenda Ivi tumeambiwa ni saa 13, bado safari ya kuitafuta Poland, tupo kama Watanzania 50 hivi kwenye hii Treni" - Nenyo.
Story Credit: Millard Ayo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable