Wadau wetu wengi wa Msasa Online wamekuwa wakitaka kujua chanzo cha yale yanayoendelea huko Ukraine basi tumefanya jitihada kuhakikisha tunakujuza kwa uzuri juu ya hili na hapa tunakusogezea andiko hili fupi karibu usome.
Fahamu kuwa kama ilivyo Urusi, Ukraine ni nchi ya Ulaya Mashariki. Kabla ya mwaka 1991, nchi zote mbili zilikuwa ni sehemu ya Umoja wa Kisovieti. Ukraine ni nchi iliyopo Barani Ulaya, idadi ya watu wake inakadiriwa kuwa milioni 44. Urusi ndio nchi kubwa zaidi duniani, idadi ya watu wake ni milioni 144.
Baada ya kuvunjika Umoja wa Kisovieti (Muunganiko wa nchi mbalimbali zikiwemo Urusi na Ukraine huko Ulaya Mashariki) Ukraine iliweka utegemezi na kufanya biashara na nchi za Magharibi ambao ni Marekani na washirika wake.
Kitendo hiki kimekuwa kikiiudhi Urusi ambayo inaona kwamba Ukraine kuwa karibu na nchi za Magharibi inaathiri usalama wake na maslahi yake.
Mwaka 2014, Rais Viktor Yanukovych wa Ukraine aliondolewa madarakani na kukimbilia uamishoni Urusi.
Huyu Rais Yanukovych alikuwa mshirika mkubwa wa Urusi, na wakati wa utawala wake alifanya mambo mengi kuipendelea Urusi.
Sasa Baada ya Rais huyo kuondolewa madarakani, Urusi ilivamia na kuiteka sehemu ya Ukraine, Crimea na kuifanya sehemu yake.
Pia baada ya Yanukovych ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Urusi kuondolewa madarakani Ushirikiano wa Ukraine na Umoja wa Ulaya umeongezeka zaidi na ushirikiano huo umeimarishwa zaidi baada ya Rais wa sasa wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuingia madarakani jambo linamuudhi sana Urusi chini Rais Putin.
Zelenskyy, Msomi wa sheria, ambaye aligeukia uigizaji na ucheshi, alichaguliwa kuwa Rais wa Ukraine mwaka 2019.
Siku chache tu baada ya kuchaguliwa ziara yake ya kwanza ya Rais huyu alitembelea makao makuu ya Umoja wa Ulaya na NATO. Urusi anaudhika kwa haya matendo. Sasa Urusi imeamua kuingia vitani ili kuzuia ushirikiano zaidi kati ya Ukraine na Umoja wa Ulaya, NATO pamoja na washirika wao ikisema Ukraine anakiuka mkataba wa Amani na Urusi.
Jana Rais Zelenskyy amesema anajua lengo namba moja la Urusi ni kutaka kumfilisi yeye mwenyewe pamoja na familia yake. Mpaka sasa watu 137 wakiwemo wanajeshi na raia wa kawaida wa Ukraine wamefariki kufuatia mashambulio ya Urusi katika nchi hiyo. Rais Zelenskyy amesema, "Ukraine iko imara na wako tayari kwa chochote kile".
Pasina shaka mdau wetu umepata kitu juu ya kile kinachoendelea huko Ukraine tafadhali endelea kuw
