RAIS WA URUSI ATAKA JESHI LA UKRAINE LIMUONDOE RAIS MADARAKANI......

0

 


Rais wa Urusi Vladimir Putin amelitaka Jeshi la Ukraine kumuondoa Rais wa Nchi hiyo Volodymyr Zelensky na Serikali yake madarakani.
 
"Nawaeleza wanajeshi wa Ukraine kwa mara nyingine tena, usiruhusu Neo-Nazis na Banderites kutumia watoto wenu, wake zenu na wazee kama ngao zao.
 
"Chukueni mamlaka mikononi mwenu mwenyewe. Inaonekana kama nyie na sisi tunaweza kupata suluhu kirahisi kuliko genge hilo la waraibu wa madawa ya kulevya na Neo-Nazis huko Kyiv." Amesema Putin akihutubia baraza la usalama nchini humo."
 
Wakati hayo yakiendelea vikosi vya Urusi vinazidi kuingia kwenye mji mkuu wa Kyiv huko Ukraine.
Hatua hii ya Putin inatajwa kama njia kuivuruga Ukraine kuanzia ndani kwa kufarakanisha Jeshi na Serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable