Hatua Sita (6) za kushika hatamu ya Maisha yako

0


 Wakati unapochukua hatamu juu ya maisha yako, ni wakati ambao wewe unakuwa kiongozi wa maisha yako. Kwa kushika hatamu juu ya maisha yako wewe ndiye unayekuwa mwajibikaji, mpangaji, na mwamuzi mkubwa wa maisha yako. Na hii ni sawa na kuwa rubani katika ndege ambapo unakuwa na ramani tosha ya kule unapotaka kwenda kwa kuanzia hapo ulipo.

Unakuwa mtu wa malengo, na unachukua uelekeo wowote ambao kwa namna moja ama nyingine unapaswa kukufikisha katika lengo lako. Kushika hatamu ya maisha yako ni moja ya uamuzi bora unaoweza kuufanya sasa. Kuna manufaa kadha wa kadha ya kuchukua hatamu ya maisha yako, na baadhi ya manufaa hayo ni kama vile; kunakusaidia kupata kile unachokitaka, kuwa mtu mwenye nguvu na uzalishaji, afya njema,matumaini,njozi,na hata kuwa na uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali katika maisha yako.Na kuna hatua za msingi unazopaswa kuzifuata ili kuanza kuchukua hatamu ya maisha yako.Na hatua hizo ni kama zifuatazo..

1.Fahamu kile kinachokupa motisha au unachopenda sana kufanya.
Hatua ya kwanza ya kuchukua hatamu ya maisha yako  ni kwa kufahamu  kile unachopenda sana kukifanya. Fahamu kile kinachokupa motisha sana kwa wewe kutaka kukifanya.Hii ni hatua ya muhimu na ya msingi inayopaswa kuzingatiwa.Na ikiwa unashindwa kufahamu ni nini hasa unachopenda kukifanya, basi ni muhimu ukatenga muda katika kufikiria na kutafakari kuhusiana na kile unachokipenda. Na kwa kuanzia, orodhesha aina zote za shughuli unazopenda kuzifanya, au ambazo ukizifanya huwa unajisikia vizuri.

2. Weka malengo yako.
Mara baada ya kufahamu kile unachopenda kukifanya, hatua inayofuatia ni kuweka malengo. Malengo yatakusaidia kuweza kupata kile unachokitaka.Malengo yanakupa hamasa na kukufanya ukazie fikra zako kwenye shauku zako. Anza sasa kujiwekea malengo yako. Malengo yanaweza kuwa ni ya muda mfupi au mrefu.Na malengo yako yanapaswa kugusia kila eneo la maisha yako kama vile; kazi, afya,fedha,mahusiano, na ukuaji wa kiroho. Andika malengo unayotaka kuyafanikisha kwenye kila eneo na uweke juhudi zako kwenye kile unachokitaka. Anza sasa kuweka malengo.

3. Chukua hatua.
Kuwa na malengo bila ya kuchukua hatua ni sawa na kazi bure.Malengo bila vitendo huwa yanapoteza thamani yake.Malengo bila vitendo hayana thamani. Safari ya maili kadhaa huwa inaanza kwa kupiga hatua.Weka malengo yako na uwe na utahayari wa kuyaendea. Fanya jambo fulani kila siku litakalokuweka karibu na malengo yako.

4. Simamia muda wako vizuri.
Muda wako una thamani kubwa sana.Muda ni rasiliamali isiyoweza kurudi tena pale inapotumiwa .Ni muhimu ukasimamia muda wako vizuri kwa kuwa na vipaumbele. Mafanikio yako ya baadae yatakuja kuamuliwa na jinsi unavyoutumia muda wako sasa. Chochote unachokipanda sasa kwa kutumia muda wako ndicho ambacho utakuja kuvuna baadaye.Ipange siku yako na ujiwekee vipaumbele kwenye muda wako.Kamwe usikubali kuupoteza muda wako kwenye mambo yasiyo na manufaa kwako.

5.Fanya kile kinachohitajika kufanyika.
Hatua ya tano ya kuweza kushika hatamu ya maisha yako ni kwa kufanya kile kinachohitajika kufanyika.Fanya kile kinachopaswa kufanywa ili kiweze kukufikisha kule unapotaka kwenda. Haijalishi ni kazi ya aina gani,wewe fanya tu kile kitakachokufikisha kwenye lengo lako.

6. Nidhamu binafsi.
Nidhamu binafsi ndio hatua ya mwisho ambayo inakusanya yote yale uliyojifunza na kuyaweka katika vitendo. Hii ni moja ya sifa muhimu na ya msingi ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuiendeleza.Ili kuweza kufanikisha malengo yako unahitaji kuwa na nidhamu binafsi.Uwe na utahayari wa kufanya kile unachopaswa kufanya hata kama haujisikii kufanya. Nidhamu binafsi ndio daraja lililopo kati yako na malengo yako.Nakutakia utekelezaji mwema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable