Mwanamitindo kutokea nchini marekani Kim Kardashian ameweka wazi juu ya kutaka talaka kwa mumewe Kanye West Baada ya kupata mfadhaiko wa kihisia kutoka kwa Rapa huyo kupitia mitandao ya kijamii, Akimsihi hakimu kutoa talaka na kutangaza kuwa yeye kwa sasa si mke tena wa Kanye.
Hii ni baada ya wanandoa hao mashuhuri wenye ushawishi na nguvu zaidi kushindwa kuwa na maelewano mazuri, februari 19, 2021 wazazi wenza hao walianza rasmi mchakato wa talaka, ambapo Kim aliwasilisha rasmi kesi ya talaka kutoka kwa mumewe.
Miongoni mwa visa vilivyobainishwa kuwa chazo cha wawili hao kutalakiana ni wivu kama tunavyojua wivu ni sababu kubwa zaidi ambayo inasababisha kuvunja mahusiano ya kimapenzi ya wasanii wengi Duniani.
Kuwepo kwa mapenzi na historia ya zamani ya wawili hao suala la talaka, Kim alitaka kuliondoa kutokana na msingi mzuri na thabiti na upendo mkubwa uliokuwepo baina yao ukisindikizwa na watoto wao.
Mnamo februari 4, 2022 Kanye amevuma kwenye mitandao ya kijamii kwa kumtuhumu mzazi mweza kuwa alimlazimisha kupima madawa ya kulevya hali iliyopelekea Kim kuamua kumfuta mumewe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Ugomvi baina yao umeendelea baada ya Kanye kuingilia kati suala la mwanae kuonekana kwenye mtandao wa Tik Tok ikiwaonyesha video fupi kati yake north west na mama yake.
Hakika ugomvi mkubwa kati ya Kim na Kanye umekuwa ukioneshwa hadharani kwenye mitandao ya kijamii, ambapo Rapa huyo amekuwa akiweka picha kwenye srini zikiwa ni meseji alizotumiwa na mtalaka wake na kwenda vitani zaidi na mpenzi wake mpya wa Kim Kardashian (Pete Davidson)
Kim kumuomba Kanye kutengana kwao kuwe kwa faragha, alishidwa kufanya hivyo na kulazimika Kanye kuwasilisha nyaraka mahakamani akitaka kupinga ombi la mkewe kutangazwa kuwa si mke tena wa Kanye West.
Wewe kwa upande wako unalizungumziaje hili suala la talaka kati ya Kim na Kanye? achia comment yako
