#MsasaUpdates MAMA ALIYEMPA AHADI YA MILIONI 4 MWANAE ASITUMIE MITANDAO YA KIJAMII MIAKA 6, SASA IMEFIKA AMPA CHAKE....
Na mwandishi wetu Nassoro Nangi.
Iwapo mtu atasema atakulipa pesa zaidi ya dola za Marekani dola $1,800 (Zaidi ya shilingi milioni 4 za Tanzania) ili kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa miaka sita, ungeweza kufanya hivyo?
Mnamo 2016, Mwanamama Lorna Goldstrand Klefsaas alimpa changamoto mwanawe Sivert raia wa Marekani aliyekuwa na umri wa miaka 12 kutotumia mitandao ya kijamii hadi afikishe umri wa miaka 18.
Ikiwa angemaliza vyema mtihani huo, angemtunza pesa Milioni 4 alizo ahidi kuwa atampa siku yake ya mfanano wa kuzaliwa atakapo timiza miaka 18 na sasa miaka 6 imepita na Februari 19, 2022 ilipofika Sivert alidai tuzo yake.
Lorna alivutiwa na mtihani huo alipousikia kwenye redio ukiitwa "16 kwa 16", ambapo mama alimpa binti yake dola za Marekani $1,600 alipofikisha umri wa miaka 16 kwa kukaa nje ya mitandao ya kijamii.
Kijana Sivert alisema haikuwa vigumu sana kuishi bila mitandao ya kijamii, na hakuifikiria sana katika kipindi cha miaka sita. Akiwa na umri wa miaka 12, Sivert alisema hakuwa akitumia sana mitandao ya kijamii. Programu pekee aliyokuwa nayo kabla ya dau kutajwa ilikuwa Snapchat ambayo aliifuta siku moja baada ya kuijaribu.
"Nisingesema kuwa kuna wakati nilidhani nilikuwa karibu kusimama," alisema. "Ilipoendelea, ilikuwa ni jambo la kujivunia."
Pia alikuwa na marafiki zake wa kumhabarisha kuhusu habari zinazojili.
Lorna alisema hakuwahi kutafuta programu zozote zilizopakuliwa (download). "Yeye ni mshindani sana, alikuwa dhahiri zaidi kwa kuthibitisha uhakika," alisema. Pia alikuwa na wakati zaidi wa kuzingatia alama zake kwenye michezo badala ya mitandao alisema Sivert
Sasa kwa pesa hizo alizopewa zaidi ya shilingi milioni 4 za Tanzania , Sivert amesema kuwa hajafikiria nini cha kununua na alipokuwa na umri wa miaka 12, alitania kwamba atapata nyumba, lakini labda inaweza kuwa sawa kwa kununua kitu cha chumbani kwake anapolala huko Chuo Kikuu cha Northwestern St. Paulo.
Lakini tayari ameamua juu ya ujio wake wa kwanza kwenye mitandao ya kijamii kwa kuanza kutumia Instagram.
"Hakika kuna njia ya kujifunza," Sivert alisema. "Ninaona marafiki zangu wakipitia programu zao za mitandao ya kijamii na siwezi kufanya hivyo bado."
Baada ya mafanikio ya Sivert, Lorna, aliingia kwenye Facebook ili kushiriki mtihani huo. Alisema ni baadhi ya pesa bora alizowahi kutumia. Wazazi wengine wameonekana kutaka kujaribu pia.
Vipi wewe utamruhusu mwanao atumie mitandao ya kijamii akitimiza umri gani?
Usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari nyingi zaidi saa 24.
