Mahakama nchini Pakistani imemuhukumu adhabu ya kifo mwanaume mmoja kwa kosa la kumbaka na kumuua binti wa mwanadiplomasia wa zamani, ambaye alikataa ombi lake la kuolewa.
Noor Muqaddam, aliyekuwa na umri wa miaka 27, alipigwa, kubakwa na kukatwa kichwa na Zahir Jaffer, ambaye ni mtoto wa miongoni mwa familia tajiri zaidi nchini Pakistan.
Mauaji hayo ya kikatili yalifanyika nyumbani kwake tarehe 20 Julai mwaka jana. Picha za CCTV zilimuonesha akijaribu kutoroka bila mafanikio.
Mauaji hayo yalizua taharuki nchini kote na kusababisha madai
ya kutaka jitihada zaidi kufanywa ili kuhakikisha usalama wa wanawake unakuepo.
