Mwandishi wa vitabu 'aliyeteswa' ataoroka Uganda - wakili

0


 

Mwandishi wa Uganda Kakwenza Rukirabashaija, ambaye ameshutumu mamlaka kwa kumtesa alipokuwa kizuizini, ametoroka nchini, wakili wake ameithibitishia BBC.

Wakili huyo hakufichua alikokwenda mwandishi huyo aliyeshinda tuzo hiyo, ambaye alikuwa amepewa dhamana na mahakama.

Rukirabashaija alikuwa ameomba ruhusa ya kuondoka nchini kutafuta matibabu kutokana na majeraha ambayo anasema aliyapata wakati alipokuwa kizuizini hivi majusi katika eneo lisilojulikana.

Lakini mahakama ilikataa kumpa mwandishi huyo paspoti yake.

Rukirabashaija alikamatwa mwezi Disemba na kushtakiwa kwa mawasiliano ya kuudhi kwa kutoa matamshi yasiyofurahisha kuhusu Rais Yoweri Museveni na mwanawe kwenye Twitter.

Katika moja alimwita mtoto wa rais - Jenerali wa jeshi Muhoozi Kainerugaba - "mnene".

Kesi yake inatarajiwa kuanza Machi 23.

Rukirabashaija anajulikana zaidi kwa The Greedy Barbarian, riwaya ya kejeli ambayo inaelezea ufisadi wa hali ya juu katika nchi ya kubuni, na Banana Republic: ambapo kuandika ni uhaini

Kitabu hicho kinaelezea mateso aliyopitia akiwa kizuizini miaka miwili iliyopita.

Mwaka jana, alijishindia Tuzo ya Pen Pinter kwa kuwa mwandishi jasiri wa kimataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable