Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 10.02.2022: Haaland, Pochettino, Diaz, Rudiger, Bissouma, Martial, Akanji

0


 

Mkufunzi wa Borussia Dortmund Marco Rose anasema mazungumzo ya "kweli" yanafanyika na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akiamua la kufanya kuhusu mustakabali wake. (Bild, via Mirror)

Wachezaji kadhaa wa Manchester United wanataka klabu hiyo kuongeza juhudi za kumteua meneja wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino kama kocha ajaye wa klabu hiyo ya Old Trafford. (Express) 

 

Baba yake winga wa Colombia Luis Diaz anadai kusita kwa Tottenham kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuliwaruhusu Liverpool kuwashinda hadi kumsaini mtoto wake. (Blu Radio,via Metro) 


 

Chelsea imempa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Antonio Rudiger mkataba mpya wenye thamani ya karibu pauni 200,000 kwa wiki katika jitihada za kumbakisha beki huyo mwenye umri wa miaka 28 Stamford Bridge baada ya kupokea ofa za kabla ya mkataba kutoka Real Madrid na Paris St-Germain ili ajiunge nao. Kwa mkataba wa bure katika majira ya joto. (Goal)

Brighton wanaweza kutarajia kufufua nia ya Aston Villa kumnunua kiungo wa kati wa Mali Yves Bissouma, 25, msimu huu baada ya kukataa dau la pauni milioni 35 katika dirisha la uhamisho la Januari. (Athletic) 


 

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 26, anasema Barcelona na Juventus walikuwa na nia ya kumsajili Januari lakini "kipaumbele" chake kilikuwa kujiunga na Sevilla kwa mkopo kutoka Manchester United. (Diario de Sevilla,via Mail)

Meneja wa Manchester United Ralf Rangnick ana nia ya kumsajili mlinzi wa Borussia Dortmund na Uswizi Manuel Akanji, 26. (Sport1,via Teamtalk)

Mlinda mlango wa Newcastle United Martin Dubravka, 33, alikataa kuhamia Manchester United kwa mkopo mwezi Januari, huku Magpies wakimpa mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovakia kwa klabu hiyo ya Old Trafford katika jitihada zao za kumnunua mlinda mlango wa Uingereza Dean Henderson, 24, hadi mwisho wa msimu. . (Manchester Evening News)

Tottenham wanaweza kumrejesha Christian Eriksen katika klabu hiyo kutoka Brentford baada ya kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye umri wa miaka 29 kwa mkataba wa miezi sita baada ya mkataba wake na The Bees kukamilika. (Guardian) 


 

Arsenal ilikataa ofa katika dirisha la usajili la Januari kwa kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny kutoka Newcastle, Leeds na Watford, licha ya kwamba kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 inatamatika Julai. (Sun)

Everton walifurahishwa na mazungumzo na mkurugenzi wa zamani wa ufundi wa Tottenham Steve Hitchen na wanaweza kumleta kama mkurugenzi wao wa kandanda. (Mail)

Mlinda mlango wa Kiitaliano Gianluigi Buffon, 44, kwa sasa anachezea Parma inayoshiriki Ligi ya Serie B lakini 'atazingatia' kuhamia Ligi Kuu ya Soka. (90 Min)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable