RAIS WA UKRAINE ATANGAZA KUGAWA SILAHA KWA RAIA YOYOTE ANAYETAKA KUPAMBANA NA URUSI.......

0

 

Mara baada ya Urusi kwenda kuivamia Ukraine hatimae Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amejitokeza kwenye vyombo vya habari akiwa nyumbani kwake na kuongea moja kwa moja na wananchi wake na kuwaambia watulie wasihofu huku akiahidi kugawa silaha kwa wananchi wake
 
Rais Zelensky amewaahidi watu wake kuwa lazima waishinde vita hiyo huku serikali ikitoa ufadhili wa silaha kwa wananchi waliotayari kujitolea kukabiliana na madui kwa lengo la kulinda taifa lao. huku akiwaasa pia wananchi wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia damu zitakazowasaidia majeruhi kwenye hospital mbalimbali .
 
Pamoja na watu kuombwa kutulia ndani ya nyumba zao misururu mirefu ya magari imeonekana barabarani wakati watu wakijaribu kuondoka katika Mji Mkuu wa nchi hiyo Kiev huku Umoja wa ulaya ukikiri kuwa huu ndio wakati mgumu kwa Ulaya tangu vita ya pili ya dunia kuisha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable