Naibu Kamishna huduma za shirika , Needpeace Wambuya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo(Happy Lazaro)
**********************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Zaidi ya wananchi 5,000 wanaozunguka
mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wanatarajiwa kunufaika na mradi wa
chujio la kutibu maji unaotekelezwa na mamlaka hiyo katika eneo la( Mama
HHau )wilayani Karatu mkoani Arusha.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Naibu
Kamishna huduma za shirika ,Needpeace Wambuya wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo ambao unatarajiwa
kuwanufaisha watalii wanaoingia katika hifadhi hiyo pamoja na wananchi
kwa ujumla.
Amesema kuwa ,mradi wa teknolojia hiyo ya kisasa
itaruhusu kiwango cha lita 1.5 milioni kutibiwa kwa siku kiasi
ambacho kitatosheleza mahitaji ambapo hadi kukamilika unatarajiwa
kutumia shs 859,000 milioni na kwa Sasa hivi umefikia asilimia 85 .
Amesema kuwa,maji yalikuwepo lakini kadri muda
unavyozidi kwenda yamekuwa yakipungua ubora kutokana na changamoto
mbalimbali ikiwemo mazingira na wanyama ,hivyo ikawalazimu kuyatibu ili
kufikia viwango vya kimataifa.
“mradi huu ulianza Septemba mwaka Jana na
unatarajiwa kukamilika june mwaka huu,na mbali na kuwanufaisha wananchi
hao pia utaisaidia hospitali ya kilutheri Karatu ambayo imekuwa
ikiwahudumia wananchi mbalimbali “amesema .
Naye Meneja wa usimamizi wa mradi huo,Godlove
Sengele amesema kuwa ,kuwepo kwa mradi huo kutamaliza tatizo la ubora
wa maji katika maeneo ya lango la Loduare,mahoteli ya kitalii,makao
makuu ya NCAA, hospital ya kilutheri Karatu,pamoja na wananchi na hivyo
kuweza kutoa huduma hiyo kwa viwango vinavyokubalika kitaifa na
kimataifa.
“Mradi huu unajengwa ili kuboresha ubora wa maji
yaliyokuwa yakitumiwa huku akiwataka wananchi watarajie maji yenye
ubora ambao unatambulika na WHO na TBS na kuweza kutambulika
kimataifa.”amesema Sengele.
Nao baadhi ya wananchi ,Neema Mollel
wakizungumza kuhusiana na mradi huo,wamepongeza kuwepo kwa mradi huo
kwani utawasaidia sana kuondokana na changamoto ya maji ya uhakika
ambayo hayachafuliwi na wanyama kutokana na kuchunjwa kabla ya kuwafikia
wananchi.
